2015-05-17 15:17:00

Papa na Rais Abbas wa Palestina waonyesha matumaini mapya


Siku ya Jumamosi , Papa Francisco alikutana na  Rais wa Palestina Mahmoud Abbas, aliyefika Vatican kwa ajili ya kushiriki katika Ibada ya kutajwa wazawa wa Nchi yake kuwa Watakatifu. Papa na mgeni wake wakikutana,katika mazungumzo yao  walionyesha matumaini yao, kwa hatua mpya zilizoanza katika mazungumzo ya amani kati ya Palestina na Israel, hasa wakitegemea maamuzi jasiri kwa ajili ya amani, kwa msaada wa jumuiya ya kimataifa.

Aidha katiak mahusiano ya Vatican na Mamlaka ya Palestina, kila upande ulionyesha  kuridhika  na makubaliano yaliyofikiwa mpaka sasa  katika rasimu ya maandishi ya makubaliano ya kina kuhusu masuala muhimu ya maisha na shughuli za Kanisa Katoliki nchini Palestina, ambayo itakuwa saini katika siku za usoni. "Rais Mahmoud Abbas , alitoa shukurani zake za dhati kwa Papa Francisco kwa kuwataja raia wa Palestina katika daraja la Watakatifu.

Pia Jumamosi Patriaki  Fouad Twal ,  baada ya kuwasili Roma kwa ajili ya tukio hili alisema , katikati ya matatizo na changamoto nyingi zinazowakabili,  kutangazwa kwa  Watakatifu wawili, raia wa  Palestina linakuwa ni tukio muhimu la kiroho, kwa  wakazi wa Nchi Takatifu.  Alionyesha imani yake kwamba,, linawakilisha mwanga mpya  katika njia yao ya Imani.  Na aliwaomba Watakatifu wapya wawili Mtakatifu Maria Ghattas na Mtakatifu Maria Baouardy , wawaangazia wakazi wa Nchi Takatifu moyo mpya kaika jinsi ya kukabiliana na changamoto ngumu zinazowakabili, ili eneo la Nchi Takatifu pawe mfano wa eneo lenye utulivu na amani .

Aidha Patriaki Twali alisema, utakaso wa wanawake wawili kutoka Mashariki ya Kati, kati ya hali hii ngumu, ni ombi jipya la  Papa Francisco, kwa Mkoa wa Mashariki ya Kati kurejesha amani, kwa kuwa ni tu  sala zinazoweza  kusaidia mkoa huo ,kuondokana na majanga ya vurugu na kutoaminiana katika njia za miujiza. Aliongeza: "Kwa sasa  wana  Watakatifu wawili wapya mfano wa ukamilifu kwa Wakristo vilevile Waislamu na Wayahudi , kwa wote wawili wanatambua  ukuu wa jina la Mariamu katika  dini  hizi tatu. Ni  ishara kwa ajili ya wakati wetu na ina  maana kubwa kwamba dini kuu tatu zinaweza kuishi na  kuwasiliana pamoja bila ubaguzi. 








All the contents on this site are copyrighted ©.