Baraza la Maaskofu Katoliki katika Jamhuri ya Kisiwa Malta, limetoa tamko lake la kichungaji juu ya utaalam wa kupandikiza viungo vya mwili kwa wahitaji, na onyo kwamba, kamwe huduma hiyo isiwe uwanja wa biashara ya viungo. Msimamo wa Maaskofu, umo katika hati ya Kichungaji ya Maaskofu iliyowasilishwa katika mkutano wa pamoja wa viongozi wa dini na wataalamu katika uwanja wa dawa na tiba, wanasaikolojia, wanafalsafa na wanateolojia.Mkutano ulioitikia wito wa Serikali, na wadau wote wa kijamii , kutoa maoni yao katika vipengere muhimu vinayohusika na maendeleo na uundaji wa sera ya afya , hasa kwa ajili ya upandikizaji wa viungo vya mwili kwa wahitaji.
Hati ya Kichungaji ya Maaskofu ilitoa msimamo wake katika vipengere kadhaa, ikianza
na Sera sasa, juu ya upandikizaji wa viungo na vikonyo vya chembe hai, ikilinganisha
na maamuzi ya nchi nyingine wanachama wa Umoja wa Ulaya. Kwa mujibu wa utafiti wa
hivi karibuni, Malta inashika nafasi ya pili katika utoaji wa viungo . Aidha, takwimu
zinaonyesha kwamba mfumo wa sasa unafanya kazi vizuri na hutoa msingi wa utendaji
unaofaa kwa ajili ya maendeleo zaidi juu ya huduma hii. Hivyo Maaskofu wa Malta wameshauri
, sheria yo yote mpya juu ya huduma hii iwe ni kuboresha badala ya kubadili mfumo
wa sasa.
Pili Maaskofu wamehimiza kwamba, uamuzi wa mtu kuchangia viungo au kiungo kwa ajili
ya kusaidia mhitaji , iwe ni kitendo cha huruma upendo na ukarimu na si kamwe isifanyike
katika mfumo wa kibiashara. Mtu hawezi kupokea kama zawadi kutoka kwa wengine, iwapo
zawadi hiyo haitolewi kwa moyo wa hiari na uhuru kamili. Zawadi ni kitu kinachotolewa
kwa ridhaa ya bure, na si utoaji ni nipe nikupe, au katika mitazamo ya kuzalisha
faida. Kutafuta faida ni kuwa kinyume na maadili.Hati hiyo imekumbusha kwamba, tangu
mafanikio ya kwanza ya tiba ya kupandikiza viungo katika miaka ya hamsini mwanzoni,
Kanisa Katoliki limesaidia kutoa mchango wake wazi unaounga mkono huduma hii kutoka
kwa aidha kwa mtu aliye hai au kutoka kwa Marehemu , lakini daima katika msisitizo
kwamba, ni lazima viungo vitolewe katika mazingira ya kweli ya haki na kanuni ya upendo
na mshikamano.
Tatu mchango wa Maaskofu umekazia masuala ya Maadili, kwamba, ni lazima dhana ya umiliki
wote wa viungo ibaki kuwa ni maamuzi binafsi yasiyolazimika kuwa na sheria mbadala
katika mifumo ya sera za kiserikali , kwa kuwa mwili wa mtu, ni binafsi, ambao hauwezi
kutegemea maamuzi ya kisemrikali , lakini basi iwapo unatolewa kwa manufaa ya wengine
linakuwa ni jamb o binafsi linalopokelewa kamazawadi kwa wengine na si shuruti . Kwa
maana hiyo viungo vyote vinavyotolewa kwa sababu za uadilifu si kitu cha kufanyiwa
biashara.
Maaskofu wameeleza katika hati yao ya kichungaji huku wakionyesha kujali kwamba,
Mfumo mbadala unaweza haribu haribu asili ya mchango wa zawadi hiiya kiungo inayotolewa
kama zawadi kwa mtu muhitaji. Na hivyo kuondokana na kujenga hofu katika akili za
watu juu hili, ni vyema kuhakikisha serikali inachukua hatua zinazofaa katika haki
miliki ya viungo na mwili wa kila mtu. Na hivyo uvunaji wa viungo kutoka watoto
wanaozaliwa, si hoja inayoibua uwajibikaji mkali wa kimaadili..
Mwisho Maaskofu walikamilisha kwa kutoa mapendekezo yao kwamba, dhana ya utoaji wa
viungo , ni lazima iwe katika mtazamo wa zawadi ya hiari, kama jambo linalotakia kulindwa
na kudumishwa. Hivyo, sheria mpya lazima ziimarishwe katika mtazamo huo. Hati inatoa
msimamo huo thabiti kwa ajili ya hatua zote zitakazojalidiliwa kwa lengo la kutaka
kuboresha mfumo mbadala, au usimamizi wa Maoni kwa ufanisi zaidi au marekebisho
zaidi .
All the contents on this site are copyrighted ©. |