2015-05-15 15:24:00

Papa amekemea Jumuiya ya Kikristo kuwa na woga na hofu


Baba Mtakatifu Francisko amekemea jumuiya ya Kikrito kuwa na woga na hofu katika kuiishi imani yake kwa Kristo akisema ,  Jumuiya hiyo yenye  woga  na isiyokuwa na furaha, inayoumwa na si jumuiya ya Kikristo, Papa alieleza katika mahubiri yake ya Mapema Ijumaa hii wakati akiongoza Ibada ya Misa katika Kanisa dogo la Mtakatifu Marta Vatican.   

Homilia ya Papa ilitafakari maneno makuu mawili :"Hofu" na "Furaha", yaliyokuwa katika liturujia ya siku.  Papa ameitaja tabia ya kuwa na hofu kwamba huongoza katika kutenda maovu.Huleta udhaifu na humrudisha muumini nyuma, na hata hupoozesha juhudi zote zake katika imani. Mtu mwenye  hofu, hawezi fanya chochote kwa kuwa hajui la kufanya na hivyo humwongoza katika utendaji wenye ubinafsi na  matokeo yake ni kutia ngiza kila jambo.  Mkristo mwoga ni mtu ambaye bado hajaelewa ujumbe wa Yesu.

Kwa ajili hii Yesu alimwambia Paulo, 'Usiogope’, kwa kuwa tabia ya woga si  tabia ya Kikristo. Kwa maneno mengine Papa anasema, woga ni kuwa na  roho aliyefungwa , Roho isiyokuwa huru, uhuru wa  kutazama maendeleo ya  mbele au  kutenda mema . Na hii ni hatari na tabia mbaya. Kwa Mkristo. Papa ameeleza na kuhoji kwa nini Mkristo awe na woga wakati  kuna silaha ya neema ya ujasiri kutoka kwa Roho Mtakatifu , mwenye kuwapatia Wakristo ujasiri ?

Maelezo ya Papa juu ya woga au  hofu pia yaliweka bayana tofauti iliyopo katika kuongopa ukuu na utakatifu wa Mungu, na woga wa kuogopa kumtaja Mungu mbele ya watu. Tofauti iliyopo kati ya woga wa kuwa mbele ya Bwana katika kuabudu na woga uadilifu wa Mungu, na woga wa kumwogopa binadamu mwingine katika kueleza hisia za imani toka ndani ya moyo. Papa alifafanua, kumwogopa Mungu, hakudhoofishi, wala kuipoozesha imani, lakini hutusaidia kusonga mbele na utume unaotolewa na Kristo katika neno lake,  na hakuna mtu atakayeiondoa  furaha hiyo kwa muumini, kama Yesu alivyosema wakati wa saa ya maumivu na mateso, kinakuwa ni kipindi cha furaha na amani.  Furaha hiyo hugeukuwa kuwa amani. Na hivyo  Mkristo anayeishi katika huzuni na woga daima huyo si Mkristo.

Papa aliendelea kuitafakari  furaha ya Mkristo, akieleza kwamba, si furaha nyepesi ya  kufuraha mambo ya kidunia,na wala siyo furaha ya mpito wa muda mfupi, bali ni furaha ya kudumu inayotoka kwa Kikristo kama zawadi,  zawadi ya Roho Mtakatifu. Ni daima kuwa na moyo wa furaha kwa sababu Bwana ameshinda, Bwana ni Mfalme, Bwana ni pamoja na Baba, Bwana ndiye anayenitazama na ndiye aliyenituma  na kunipa neema yake na mimi kama mtoto wa Baba ... Na ninafurahia kuwa Mkristo. Mkristo huishi kwa furaha. "

Papa alieleza na kuzitazama kwa makini jumuiya inayoishi bila furaha akiitaja jumuiya  kamahiyo inamatatizo,inaumwa, imesongwa na maradhi,kwa kuwa imejenga msingi wake katika mambo ya kidunia . Na ndivyo ilivyo kwa Kanisa lenye woga ,kanisa hilo lina matatizo ,ndani mwake halina  Roho Mtakatifu, Ni Kanisa gonjwa, waamini wake ni wagonjwa na jumuiya hiyo ina maradhi ya kiroho" Papa inamalizika na  sala akimwomba Bwana , ashushe roho yake ili sote tuweze kuinuliwe na kuelekea alikoketi Kristo,katika mkono wa Kulia wa Baba , ainue roho zetu na kuondoa kila jambo lenye kututia hofu na woga badala yake atupatie furaha na amani yake  milele.. 








All the contents on this site are copyrighted ©.