2015-05-15 14:46:00

Miaka 25 ya uhusiano wa kidiplomasia kati ya Vatican na Romania!


Baba Mtakatifu Francisko, Ijumaa tarehe 15 Mei 2015 amekutana na kuzungumza na Bwana Klaus Werner Iohannis, Rais wa Romania ambaye baadaye amekutana na kuzungumza pia na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican aliyekua ameambatana na Askofu mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu mkuu wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa.

Katika mazungumzo hayo Baba Mtakatifu na Rais Iohannis, wamegusia kumbu kumbu ya Jubilei ya miaka 25 tangu Romania na Vatican walipoanzisha uhusiano wa kidiplomasia; tukio ambalo lilifanyika hapo tarehe 15 Mei 1990. Uhusiano huu umekuwa na mafao makubwa kwa pande zote mbili sanjari na mahusiano mazuri kati ya Serikali na Kanisa mahalia katika mchakato wa kudumisha amani na utulivu. Wakati wa mazungumzo yao, viongozi hawa wawili wamejadili pia masuala ya kimataifa na kikanda.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.