2015-05-14 15:45:00

Kanisa halina watalaam waliobobea kisayansi, lakini ni bigwa katika ubinadamu


Kardinali Peter Turkson , Rais wa Baraza la Kipapa ka ajili ya Haki na Amani , Alhamisi  hii akitoa mchango wake katika Mkutano Mkuu wa Caritas Internationalis, Mkutano uliofunguliwa rasmi kwa Ibada ya Misa Jumanne na Papa Francisko,  amegusia yote yaliyofanyika na yanayotazamiwa kwa siku za baadaye. Na akatahadharisha kwamba, Kanisa  halina wataalam waliobebea  Kisayansi au teknolojia, au uchumi, bali hutegemea watu wema,kama ilivyo kwa baadhi ya wajumbe wa Mkutano  unaoendelea. Lakini Kanisa ni mtaalam katika ubinadamu na katika utoaji wa ujumbe wa  kweli  kwa mwanadamu kutenda kwa haki na upendo.  Hivyo ni  kwa sababu hii kwamba, Kanisa huweza kujisoma ishara za nyakati, katika utabiri wa matukio muhimu kihistoria.

 Kardinali Turkson alieleza na kurejea historia ya karne ya 19 na mapema  na mwishoni mwa karne ya 20, ambamo Kanisa lilionyesha wasiwasi kina kwa ajili ya kukosekana kwa haki kulikozua mfumo wa mshikamano wa wafanyakazi viwandani, kwa uwepo wa pengo kubwa kati  wachache wenye  navyo na raia wengi  wasiokuwa navyo.  Na kwamba katika nusu ya mwisho ya karne iliyopita, Kanisa  liliangalisha katika  changamoto ya  mwiba wa maendeleo ya kimataifa, na tishio kubwa la kurundikana kwa silaha za nyuklia wakati wa vita baridi. Na kwa sasa Kanisa linazungumzia kwa nguvu changamoto za wakati wetu ,ambayo ni maendeleo endelevu na ustawi wa  binadamu ndani katika mazingira ya asilia, yanayowekwa katika hatari kubwa zaidi, ya kutokomezwa.

Kardinali Turkson , aliendelea na maelezo yake , akiangalisha pia katika tukio lijalo la mwezi Septemba, ambamo Papa Francisco anatazamiwa kulihutubia Baraza la Umoja wa Mataifa kuhusu malengo ya maendeleo endelevu, ikiwa imepita miaka hamsini, tangu Mwenye Heri  Papa Paulo VI alipohutubia pia Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa , juu ya matatizo mbalimbali yaliyokuwa yakiikabili jamii, ambayo hata leo hii Kanisa linaendelea kuwa thabiti katika ujumbe wake.  

Baba Mtakatifu Paulo VI, alitoa wito wa kuzingatiwa kwa  dhamiri ya kimaadili kwa mtu , kama ilivyokuwa muhimu kwa wakati ule, hata leo hii inaendelea kubaki  sharti msingi na muhimu, kwa ajili ya maendeleo ya kweli ya  binadamu.. N hivyo ni muhimu  kwa dunia kuwa na sera zenye kuzingatia fadhila msingi katika utetezi na mshikamano ili mazingira yabaki katika asili yake.. Amesema bila uwepo wa utetezi katika mambo msingi, sayari yetu itaendelea kuharibiwa kidogokidogo na hatimaye kushindikana kuishi ndani yake. Utetezi huu unahitaji mshikamano wa dhati wa watu wote,  kwa kuwa uchoyo na umimi huleta uharibifu mkubwa zaidi.

 Na kwa pamoja  katika njia ya utetezi na mshikamano, binadamu wote wanakuwa na uhakika wa kuanzisha na kuendeleza zaidi maendeleo endelevu yenye na usalama mkubwa zaidi. Na hivyo  binadamu wanaweza kuhudumia  kwa ukarimu tufe la dunia kama nyumbani kwa kila mmoja , wake kwa waume na  kila mtoto wa kila nchi na kila kizazi.  Na kufikia lengo hilo, tunahitaji wongofu  binafsi, kufanya upya fikira zetu, kama alivyoeleza Mwenye Heri Paulo VI, nusu karne iliyopita , na Papa Francisco daima anaendelea kuhimiza hilo.

Kardinali Turkson ameomba baraka za Mungu kwa Kanisa, waamini wote na  watu wote wenye mapenzi mema,zisaidie  kuwaunganisha  pamoja, kwa ajili kukabiliana na changamoto zinazojitokeza katika nyakati zetu.

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.