Baba Mtakatifu katika Katekesi yake ya kila Jumatano, ameendelea na Mada juu ya familia , leo akitafakari juu ya maneno matatu ya kawaida “Naomba”, "Asante", na "nisamehe ". Alianza kusema , maneno haya kawaida, kwa leo hii yanaonekana si rahisi kutamkwa na hasa kimatendo. Lakini wakati yanapopuuzwa , na kukosekana kwake katika mazungumzo ya kila siku ndani ya familia, husababisha nyufa myimgi katika msingi wa maisha ya familia, na hivyo kunaweza leta uharibifu mkubwahata familia kusambaratika. Lakini iwapo maneno haya yanakuwa ni sehemu ya maisha yetu ya kila siku, sio tu yanakuwa usemi rasmi wenye kuonyesha tabia njema, lakini pia kama ishara ya upendo kina kwa ajili ya mtu mwingine, ni maneno yenye kuimarisha maisha ya familia na furaha.
Papa aliendelea kufafanua kwa kina , neno “naomba “hata kama ni haki kupata jambo hilo, wakati tunapozungumza na wenzi wetu au familia zetu kwa upole na unyenyekevu ,mnakuwa na nguvu ya kutengeneza nafasi kwa ajili ya roho ya ukweli katika maisha ya kawaida , hasa maisha ya ndoa na familia. Neno hili "naomba " pia peke yake huonyesha upya imani na heshima, kwa wengine na huruhusu kufungua mlango wa moyo wetu kwa wengine.
Papa aliendelea na Neno "Asante" akisema, kuna haja kubwa kwa jamii yetu kuwa na moyo wa shukrani, kutoa shukurani hizo kwa neno moja tu "asante ", neno linalotufanya sisi kuona unyeti wa hadhi ya binadamu na mahitaji ya haki za kijamii. Shukrani pia ni lugha ya Mungu, ambaye zaidi ya yote,sisi sote ni lazima tunapaswa kusema Asante kwake kwa mengi mema anayotujalia bila hata kumwomba.
Papa aliendelea na neno "Nisamehe” akisema bila uwepo wake huweza umiza maendeleo katika uhusiano , hivyo kudhoofisha maisha yetu kama familia. Kwa kuomba msamaha, huonyesha hamu ya kutaka kurejesha upya kile kilichopotea katika uhusiano wetu, heshima, uaminifu na upendo. Nisamehe ni neno la uponyaji kati ya wanafamilia na lina uwezo wa kufanya hivyo.
Baba Mtakatifu alimalizia mafundisho kwa kumwomba Bwana atuwezeshe kuyaweka moyoni maneno haya "Naomba", "Asante", "Nisamehei"ndani ya mioyo yetu, katika familia zetu na jamii zetu.
Baada ya Katekesi Papa alisalimia kwa moyo wa dhati makundi ya mahujaji na wageni
waliofika kumsikiliza na wengi wao wakiwa kutoka Uingereza, Sweden, Taiwan, Cameroon
na Marekani. Aliwatakia nguvu ya Kristo iweze kuwaimarisha zaidi na zaidi imani
yao na imani kwa familia zao , ili daima ulimwengu uweze ona upendo wa Mungu na huruma
yake.
All the contents on this site are copyrighted ©. |