2015-05-11 14:56:00

Papa anasema; Siku isipite bila kuomba samahani na kupatana


Baba Mtakatifu  Francisco Jumatatu hii, amekutana na ujumbe wa watoto na vijana wapatao elfu saba mjini Vatican,  kutoka Chama kinachojulikana kama “Kiwanda cha Amani , ambacho wanachama wake ni wanafunzi mashuleni,  wenye  tamaduni na imani mbalimbali.  Chama hiki ni mradi wa elimu, unaofanikishwa kwa ushirikiano, wazazi, walimu, Wizara ya elimu ya Italia na Maaskofu wa Italia, kama njia ya kushirikishana  uzoefu na kutiana  shime bila kuchoka katika kazi muhimu za kuelimisha kizazi kipya,  kama jambo muhimu katika makuzi na mabadiliko ya akili na kwa ajili ya kuhakikisha usalama wa watoto katika dunia yetu isiyokosa marumbano,  vita na dhuluma. 

Papa, alitoa  hotuba yake kwa kujibu maswali 13 yaliyokuwa yameandikwa na watoto.Na alilenga zaidi  katika jinsi ya kufanikisha na kudumisha amani Na aliwapa uzoefu wake katika maisha ya kawaida ya familia ambamo wanafamilia hawakosi kugombana , lakini mara hupatana. Na kuhimiza siku isipite bila kuomba samahani  na kupatana .

Na hivyo akasema, kwa ajili ya utendaji mzuri zaidi kwa kazi ya  kujenga amani, inahitaji kuwa na hekima na mshikamano, tangu katika  ngazi ya chini kabisa, ndani ya mazingira ya maisha ya kila siku, ndani ya  familia, mashule,  mahakama , penye kumbi za michezo  na midahalo.   Na hivyo inakuwa ni jambo muhimu kwa wote kufanya kazi pamoja na watu wanaoishi karibu na sisi: marafiki, wanafunzi, wazazi na waalimu.  

Papa alitaja jambo jingine wanalopaswa kuzingatia katika kiwanda hiki cha amani kwamba, ni kutokuwa mipaka katika kuwapokea wenye matatizo. Ni  kuwakaribisha wote bila  vikwazo au ubaguzi wa kimbali, kikabila , kimila utaifa au dini. Wanapaswa kufanya kazi zao katika uelewa kwamba,  kujenga dunia ya amani ni maslahi muhimu katika mahitaji ya maskini, wengi kutelekezwa na mateso, hata wale walio mbali .  Na hivyo kazi za chama chao,  zinakuwa kweli kazi ya upendo. Upendo kwa  wengine, hasa wasiokuwa na uwezo zaidi, ina maana kutoa  ushuhuda kwamba , kila mtu ni  zawadi kutoka kwa Mungu.

Daima kila tendo zuri tunalolifanya liweze kuleta mabadiliko kwa mtu mwingine. Sisi sote tunahitaji mabadiliko  mazuri , kubadilika katika njia  zetu za maisha na utendaji kwa ajili ya mazuri si kwetu wenyewe tu lakini kwa ajili ya wengine pia. Kwa hiyo ni muhimu sio tu kuwa mashahidi wa amani na upendo, lakini pia mashahidi wa maombi, kwa kuwa kuomba ni  kuzungumza na Mungu, Baba yetu aliye mbinguni, na kumwambia yote  tuliyo nayo iwe  furaha au  huzuni.  Na kuomba ni kuomba msamaha kwa yale tunayo fanya makosa na kutenda dhambi yoyote, tukiwa na  uhakika kwamba Mungu  daima husamehe.

Mwisho Papa aliwashukuru wote na kuwapa Baraka zake za Kichungaji. 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.