Wauguzi duniani kote, watasherehekea Siku ya Dunia ya Wauguzi, Jumanne ijayo. Adhimisho la kila mwaka tarehe 12 Mei, ambayo ni siku ya kuzaliwa Florence Nightngale, mwanzilishi wa huduma za uuguzi. Baraza la Kimataifa la Wauguzi, limetangaza Kaulimbiu ya adhimisho la mwaka huu kuwa, Wauguzi:Nguvu ya mabadiliko,ufanisi wa huduma kwa binadamu kwa gaharama nafuu. Maadhimisho ya siku hii, yanatajwa kuwa na umuhimu wake kutokana na umuhimu ya huduma hii inayogusa maisha ya kila binadamu. Kila mwaka hufanikisha kupitia mipango mbalimbali inayoandaliwa na wauguzi mahalia. Kati ya yatakayofanyika mwaka huu, ni pamoja na usambazaji wa majarida ya elimu na habari kwa umma, juu ya huduma ya wauguzi mahali popote duniani.
Kwa ajili ya mwaka huu , tayari Baraza la Dunia la Wauguzi , limekwisha sambaza mabango yenye kuonyesha huduma ya muuguzi, kwa ajili ya kutoa ufahamu zaidi wa huduma za wauguzi katika maisha ya kijamii. Mabango yaliyotundikwa sehemu mbalimbali na vyama vya wauguzi kitaifa duniani kote. Waandaaji wa tukio hili katika ngazi ya kimataifa wanahimiza wauguzi kila mahali, kufanikisha upanuzi wa huduma za Wauguzi, kama Nguvu ya kuleta mbadiliko, katika ufanisi wa huduma kwa binadamu anayeteswa na maumivu.
Katika baadhi ya mataifa , adhimisho hili hufanyika kwa muda wa wiki moja kitaifa,ili kumulikia zaidi umuhimu wa huduma za wauguzi , kama ilivyo nchini Tanzania mwaka huu wanalenga zaidi katika huduma za wakunga , katika kupunguza vifo vya watoto wachanga na wakina mama wajawazito.
Kwa mujibu wa Shirika lisilo la kiserikali la « Evidence4Action », watoto 47,000 wenye umri wa chini ya miaka mitano wanaofariki dunia kila mwaka Tanzania, nusu ya vifo hivyo hutokea wakati wa kuzaliwa. Na kwamba licha ya Tanzania kupiga hatua kubwa kwa kutimiza lengo la Maendeleo ya Milenia namba 4 la kupuguza vifo vya watoto wachanga, bado kuna watoto wanaopoteza maisha kutokana na huduma mbovu za afya ya uzazi.
All the contents on this site are copyrighted ©. |