2015-05-08 15:19:00

Wachungaji wa Makanisa ya Kipentekoste wakutana na kusali na Papa!


Baba Mtakatifu Francisko, Alhamisi, jioni tarehe 7 Mei 2015 amekutana na kuzungumza na wachungaji wa Kanisa la Kipentekoste kutoka sehemu mbali mbali za dunia waliokuwa wameonesha shauku ya kutaka kuzungumza na kusali pamoja naye. Kundi hili lilikuwa linaongozwa na Mchungaji Giovanni Traettino, aliyekuwa ametembelewa na Baba Mtakatifu Francisko hivi karibuni na kusali pamoja.

Mkutano huu kati ya Baba Mtakatifu Francisko na wachungaji wa Makanisa ya Kipentekoste umefanyika kwenye Ukumbi mdogo wa Paulo VI mjini Vatican na kuhudhuriwa pia na Kardinali Kurt Koch, Rais wa Baraza la Kipapa linalohamasisha umoja wa Wakristo. Taarifa inaonesha kwamba, Baba Mtakatifu na wageni wake wamezungumza na baadaye wakasali kwa pamoja, katika hali ya amani, utulivu, upendo na mshikamano wa kidugu.

Na Padre Richard A, Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican. 








All the contents on this site are copyrighted ©.