Askari wawili wa Watanzania , waliokuwa wakitumikia Tume ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kulinda amani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, wameuawa, wengine 13 kujeruhiwa, na wanne hawajulikani walipo, baada ya kushambuliwa ghafla mapema siku ya Jumanne , wakiwa katika lindo. watu wanaodhaniwa kuwa waasi wanamgambo Kiislam wa Uganda,waliwashambulia askari hao, Umoja wa Mataifa umetaarifu .
Felix Basse, Msemaji wa Tume ya Kulinda Amani inayojulikana kwa jina la MONUSCO, bila kutaja majina ya marehemu amesema, askari hao walishambuliwa katika kijiji cha Kikiki, kiasi cha Km 50 (30 miles) Kaskazini mwa mji wa Beni, Kivu Kaskazini, mapema Jumanne. Na kwamba Jeshi la DRC, liliua waasi 16 wanamgambo wa chama cha Uganda Allied Democratic Forces (ADF), wakati wa mapigano makali yaliyofanyika katika ukanda huo mwishoni mwa wiki.
Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, akithibitisha taarifa za kuuawa kwa Askari hao , amesema, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amelaani vikali mashambulizi dhidi ya Walinzi wa Amani, wanayofanykazi kazi zao kwa dhamira ya kutoa ulinzi kwa raia. Na kwamba juhudi za Umoja wa Mataifa kutetea raia wema hazitakatishwa tamaa na mashambulizi kama hayo lakini umoja huo , utachukua hatua zote muhimu kulinda raia na kusambaratisha makundi ya waasi katika Mashariki mwa DRC.
Na Mkuu wa Tume ya MONUSCO, Martin Kobler, akiwa wametiwa simanzi na tukio hili, anasema, hawatavumilia tena ya mashambulizi haya mara kwa mara dhidi ya Watunza amani wilayani Beni. Na sasa MONUSCO itatekeleza shughuli zaidi kwa uimara zaidi.
Na Rwanda yajihami na wingi wa wakimbizi tokea Burundi
Na taifa la Rwanda siku ya Jumanne lilionyesha kujali wingi wa wakimbizi wanaoingia
Rwanda tokea Burundi , kufuatia maandamano ya upinzani nchini Burundi dhidi ya maamuzi
ya Rias Pierre Nkuruzinza kutaka kugombea kiti cha Rais awamu ya tatu. Upinzani mkali
ulianza baada ya Rais Pierre Nkurunziza kutangaza nia yake ya kutaka kusimama katika
uchaguzi wa Juni 26 kugombea kiti cha Rais,na hivyo kuitumbukiza Burundi katika mgogoro
mpya wa kisiasa, baada ya kuwa na utulivu na amani kwa takribani miaka kumi, baada
ya kusitishwa vita ya wenye kwa wenyewe vilivyodumu kati ya 1993-2005.
Habari inasema, kwa wakati huu ,Watu zaidi ya 24,000 wengi wao wakiwa Watutsi wamekimbilia
Rwanda, kwa hofu ya kuzuka kwa mapigano mengine ya kikabila, ambayo itakuwa ni kutonesha
kovu la Rwanda, ambayo bado inalilia watu wake waliofariki katika mauaji ya kimbari
ya 1994, yaliyoua zaidi ya 800,000 Watutsi na Wahutu. Waziri wa Mambo ya Nchi za
Nje , Louise Mushikiwabo anasema, pamoja na kuheshimu sana uhuru wa Burundi katika
kushughulikia mambo yake ya ndani, Rwanda inaona usalama wa watu wasio na hatia kimkoa,kikanda
na kimataifa, unaweka hatarini. Na hivyo wanatoa ombi kwa viongozi wa Burundi kufanya
kila linalowezekana kurudisha hali ya utulivu na amani katika taifa lao .
Kwa mujibu wa taarifa za vyama vya kiraia na kijamii, tangu kuzuka kwa maandamano ya upinzani mitaani Burundi, wiki iliyopita, watu 12 wameuawa, katika mapambano na polisi. Siku ya Jumanne makundi madogomadogo ya upinzani yalirejea tena mtaani na polisi mabomu ya machozi na mipira ya maji kusambaratisha waandamanaji. Katibu wa Nchi wa Marekani, John Kerry, akiitembelea Afrika, Jumatatu, mbele ya wanahabari, alimtaka Rais Pierre Nkuruzinza kuheshimu Katiba ya Burundi, kwani nia yake ya kutaka kutawala kwa awamu ya tatu ni moja kwa moja kukiuka katiba ya Burundi katiba.
Wakimbizi Tanzania
Wakati huohuo taarifa zimetolewa kwamba, zaidi ya wakimbizi 4000 wa Burundi wameingia Tanzania, idadi kubwa ya wakimbizi hao ni wanawake na watoto. Hllo limethibitishwa na Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Alvaro Rodriguez,wakati akizungumza na vyombo vya habari. Na kwamba kwa sasa wako katika mashauriano na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi na wahisani ili kuongeza usaidizi wa huduma za msingi kwa wakimbizi hao ikiwemo chanjo kwa watoto , ambapo serikali ya Tanzania imeshajadili suala la kutoa eneo la kujenga kambi nyingine, iwapo idadi ya wakimbizi itaongezeka zaidi.
Na Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania , kama Mwenyekiti wa sasa wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Burundi ikiwa mwanachama wa Jumuiya hiyo, amepeleka ujumbe wa mawaziri kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kutathmini machafuko ya kisiasa Burundi. .
Taarifa kutoka Ofisi ya Rais iliyosambazwa katika vyombo vya habari na Mawasiliano, siku ya Jumanne, inasema Ujumbe huo utakutana na wadau wote muhimu katika mzozo wa Burundi. Tume inatazamiwa kukamilisha kazi yake mwishoni mwa wiki. Na kwamba suluhisho la hali ya kisiasa inayoendelea Burundi, linaweza tu kupatikana iwapo Burundi itaheshimu sheria mama za nchi na Sheria ya Uchaguzi. Rais Kikwete alieleza wakati akijibu swali katika mkutano wa Umoja wa Mataifa siku ya Jumatatu mjini New York.
All the contents on this site are copyrighted ©. |