Mkutano wa siku tatu wa Wakuu wa Nchi katika Kanda Maziwa Makuu na watoa maamuzi wengine , ulifanyika kwa ufadhili wa Rais wa Jamhuri ya Congo Brazzavile, tangu tarehe 27-30 Aprili 2015, kwa ajili kupambana na Biashara haramu ya wanyama pori na mimea wanaoporwa toka barani Afrika. Mkutano huu ni mwendelezo wa juhudi zinazolenga kusalimisha uwepo wa aina zote za wanyama na mimea asilia barani Afrika. Mkutano ulibaini kwamba usafirishaji wa wanyamapori unaendelea kuwepo kutokana na uhaba wa vyombo vya ulinzi thabiti,ikishamirishwa na uwepo wa migogoro ya kisiasa na rushwa. Pamoja na ujangili huo pia kuna uchimbaji haramu wa madini unaonyonya utajiri wa Afrika bila kunufaisha wenyeji , kutokana na udhaifu katika utekelezaji wa sheria za serikali, wenye kuruhusu mgawanyiko katika jamii.
Wajumbe katika mkutano wao walisisitiza kwamba, jamii inapaswa kuwa na ufahamu
wa kutosha , juu ya madhara ya usafirishaji haramu wa Wanyamapori, pia kwamba ,
ni kuharibu viumbe hai na mazingira, na ni tishio katika upatikanaji wa chakula
na maji safi na humomonyoa maisha ya mamilioni ya watu barani Afrika.
Mkutano huu wa hivi karibuni uliandaliwa na Serikali ya Jamhuri ya Congo na Tume ya
Umoja wa Afrika (AUC), kwa kushirikiana na UNEP na Shirika la Umoja wa Mataifa la
Maendeleo (UNDP). Baada ya mkutano huu kinachofuata ni Mkutano mwingine wa 23 wa Umoja
wa Afrika , unalenga kutoa wito kwa mataifa ya Afrika , kutumia uwezo na mbinu thabiti,
katika kuchukua hatua za kuimarisha sheria na sera, na ushirikiano na jamii, kwa
ajili ya kupambana na biashara haramu ya wanyamapori na shughuli zinazohusiana na
uhalifu huo. Mkutano unalenga kujaribu kujenga mkakati wa Afrika nzima, ikihusishwa
na mpango wa utekelezaji dhidi ya biashara haramu ya wanyama pori na mimea, mapendekezo
yatakayo fikishwa katika Mkutano ujao wa AU, kwa ajili ya maamuzi zaidi ya utekelezaji.
Kati ya viongozi wakuu walioshiriki katika Mkutano wa Kimataifa wa 27-03 Aprili 2015,
juu ya Biashara haramu ya pori wanyama na mimea, uliofanyika katika Ikulu ya Congo
Brazzaville ni pamoja na mwenyeji wa mkutano Rais Denis Sassou Nguesso, pia Marais
na Wakuu wa Nchi kutoka Mkoa wa Maziwa Makuu waliokuwa wameandamana na , Waheshimiwa
Mawaziri wa Wizara zinazohusika na Wanyamapori, pia akiwepo Kamishna wa Uchumi
wa Vijiji na Kilimo wa AU, na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa UNEP, na Mratibu Mkazi
wa UN na UNDP, Mwakilishi Mkazi nchini Kongo.
Katika Mkutano huu , wajumbe walihimiza zaidi uratibu mzuri wa vyombo vya upelelezi, na utekelezaji wa sheria, wenye kuishirikisha jamii yote ya Afrika kwa kushirikiana na serikali za nchi ambako bidhaa zina soko. Wote kwa pamoja ni lazima kuwa kujenga moyo thabiti katika kuikataa biashara hii ya kutisha na kukabiliana nayo. Nchi lazima zilichukue kama dharura, inayo hitaji uratibu wa karibu wa kimataifa, ktika kukomesha ujangili na uporaji wa mali za Afrika. Ni kuwa na udhibiti mkali wa polisi, ikiwa ni pamoja na kuimarisha ukaguzi katika maeneo ya mpakani.
Rais Nguesso ameitaka jumuiya ya kimataifa ili kuendeleza ushirikiano wake katika hili na hasa uhamasishaji dhidi ya uhalifu wa mazingira na kufanya imara sheria zinazowekwa na nchi kwa ajili ya apambano dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi na changamoto nyingine duniani. Na kwamba hakuna nchi inayoweza kufanikiwa katika mapambano haya bila ushirikiano wa kimataifa.
All the contents on this site are copyrighted ©. |