2015-05-01 13:00:00

Onesho la Chakula Milano: Utandawazi wa mshikamano kupambana na njaa!


Tarehe Mosi, Mei, 2015 Maonyesho ya Kimataifa ya Expo 2015, yamezinduliwa rasmi .  Kwa ajili hii Baba Mtakatifu Francisko, alituma ujumbe kwa njia ya mawasiliano ya video  ambamo  amemwomba Bwana, amjalie kila mmoja kuwa na hekima na ujasiri wa kujali majukumu na wajibu. Na ameonyesha matumaini yake kwamba, uzoefu huu utaruhusu wajasiriamali, wafanyabiashara na  wasomi, wapate hisia kali za kushiriki  katika mradi mkubwa wa mshikamano, kwa ajili ya kulisha dunia, ili kila mwanamume na mwanamke aweze  kuishi kwa hadhi na kuheshimu mazingira ya asilia.

Uzinduzi wa Maonyesho ya Kimataifa ya Expo 2015, ulianza Alhamisi jioni  katika ukumbi mkubwa wa jiji la Milan , Kaskazini mwa Italia kwa tamasha la muziki  na uwashaji wa taa katika  mti uliopewa jina “mti wa maisha” na kufunuliwa kwa Nembo ya onyesho hilo hapa Italia. Maonyesho haya ya kimataifa yatakayoendelea hadi tarehe 30 Oktoba, yanahudhuriwa na uwakilishi kutoka nchi 145 za pande zote za dunia na yanafanyika katika uwanja wenye ukubwa wa  ekari 110, Kaskazini Magharibi mwa Milan. Tamasha la ufunguzi lilivutia umati mkubwa watu wpatao 20,000, akiwemo Rais wa Italia Mattarella .  

Baba Mtakatifu katika ujumbe wake , ameshukuru kupewa nafasi hii kuongeza sauti yake katika sauti nyingi zitakazozungumza katika tukio hili, lililokusanya watu wengi, kwamba , sauti yake kama  Askofu wa Roma, isikike kwa niaba ya watu wa Mungu  waliotawanyika  duniani kote;  iwe  sauti ya watu maskini wengi, na hata wale wanatafuta uwezekano wa  kupata chakula chao kwa jasho lao kwa heshima.  Na hivyo Papa anakuwa  msemaji wao wote wake kwa waume, Wakristo na hata wasio Wakristo, ambao wote Mungu anawapenda kama watoto wake, ambao kwao aliyatoa maisha yake,  akamega mkate, ambayo ni mwili wa Mwana wake, aliyefanywa kuwa binadamu. Mwanae aliyetufundisha kumwomba Mungu Baba , “ Utupe mkate wetu wa kila siku.  Na hivyo Maonyesho haya ya  Expo , iwe ni  fursa nzuri ya kulimwengusha mshikamano wa dunia kwa watu wote. Na akaomba nafasi hii isipotee bure bali tuitumie kwa manufaa ya watu wote. 

Baba Mtakatifu ameeleza na kuirejea Mada ya Maonyesho inayo wahimiza wote kujenga umoja kwa ajili ya ”Kulisha Sayari, Nishati ya Maisha". Na hivyo akamshukuru Mungu kwa mada hiyo kuchaguliwa akitaja kuwa ni mada muhimu na ya lazima , na sasa si tu itolewa kama mandhari" lakini daima  iongozane  utambuzi wa uwepo wa nyuso za mamilioni ya watu leo hii wanaokabiliwa na  njaa , ambao hawawezi kupata milo inayostahili kibinadamu. Na hivyo Papa ametoa wito kwa kila mtu kuanzia leo, hasa kila mtu atakayetembelea Maonyesho hayo ya EXPO Milano, kupitia mabandani  yake ya ajabu, aweze kupata hisia za uwepo wa nyuso hizo zenye njaa. Uwepo wa watu hao wenye njaa uliofichika, lakini ni ukweli halisi unaotakiwa kushughulikiwa  kikamilifu kupitia hili, nyuso za  wanaume na wanawake  walio na  njaa,  wagonjwa, na wanaokabiliwa na kifo kutokana na kukosekana kwa huduma za afya na pia maskini au madhara mengine  wanayoshindwa kuyakabili kutoka na hali yao ya umaskini. .

Papa ameeleza na kurejea hotuba iliyotolewa pia na Mtagulizi wake , Mtakatifu Yohana Paulo II alipouhutubia  Mkutano Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Chakula na Kilimo, Mkutano wa Lishe wa mwaka  1992. Akisema hata leo hii , bado balaa la njaa linaendelea kuathiri watu licha ya juhudi zinazofanywa na baadhi ya matokeo  yake mazuri. Kwa ajili ya kupata jibu katika kitendawili hiki, Papa Francisko , ameomba dunia iondokane na  utamaduni wa taka, utupaji kwa kuwa hauchangii chochote katika  maendeleo endelevu. Kwa hiyo maonyesho ya   Expo, pawe ni mahali pa kuleta mabadiliko ktiak kufikiri , kufuta fikira zisizojali athari kwa watu wengine iwe walio  karibu au mbali,  wanaokabiliwa na balaa la njaa,  wanawake wengi na  hasa wingi wa watoto , wanakufa kutokana na njaa duniani.

Baba Mtakatifu Francisco amesema,  kuna watu wengi mashuhuri watakao shiriki katika maonyesho haya ya Ulimwengu, , wakiwemo  watafiti katika sekta ya chakula. Kwao wote , Papa amewaombea kwa  Bwana , zawadi ya  hekima na ujasiri mkubwa  katika  jukumu lao. Na ameonyesha matumaini yake kwamba, maonyesho haya ya Expo yataweza kuruhusu  wajasiriamali, wafanyabiashara, wasomi, kujisikia  kuwa ni  washiriki  muhimu katika mradi mkubwa wa mshikamano wa kulisha dunia na katika kuheshimu mazingira ya asilia. Papa ameitaja hii kuwa ni changamoto kubwa ambamo Mungu anatoa wito kwa binadamu wa karne ya ishirini , kuachana na matumizi mabaya ya bustani ya Mungu, ambayo ameiweka ili kwamba , kila mtu anaweza kula matunda ya bustani hii. Kila mmoja na aone umuhimu wa kuingia katika mradi huu mkubwa, kwa heshima kamili,iwe kwa wale wanaofanya kazi za uzalishaji au wale wanaofanya utafiti  kwa ajili ya chakula.

Kutokea huko Milan, iwe ni kuzitazama nyuso za thamani za watu wahitaji, na bila kuwasahau  wafanyakazi wote wanaofanikisha onyesho hili la Milan Expo, na hasa wale ambao majina yao hayajulikani , na waliofichika zaidi . Papa ameshukuru kwa maonyesho hayo kwa kuwezesha baadhi ya watu kupata ujira wa kupeleka nyumbani, Na akaomba asiwepo mtu aliyenyimwa  hadhi hii! Na  chakula iwe ni matokeo ya kazi zinazostahili kwa kila mtu!

Papa amekamisha ujumbe wake kwa kuomba msaada wa Bwana ili maonyesho haya kweli iwe ni nafasi ya kuwajibikaji.Na kwamba Ni Kristo mwenyewe mwenye kuitoa zawadi hii ambayo ni Upendo , Ukweli na Nishati ya maisha, Upendo wa kugawana  mkate, "riziki yetu ya kila siku", kwa amani na udugu. Papa ameomba ili kwamba, asiwepo mtu wa kupungukiwa chakula na kazi ya heshima, iwe kwa mwanaume na mwanamke.








All the contents on this site are copyrighted ©.