2015-04-29 15:10:00

Papa-mwalikeni Yesu katika ndoa yenu na mtaona muujiza wake.


Kama kawaida Baba Mtakatifu Francisco , Jumatano hii ametoa mafundisho yake kwa mahujaji na wageni waliotembelea vatican kwa nia ya kusikiliza mafundisho yake.  Papa ameendelea kuizungumzia  familia, leo akiangalisha katika matatizo yanayokabili jamii ya leo katika mtazamo wa ndoa , ambamo wengi hawapendi kufunga ndoa, na wenye ndoa wanatarakiana bila sababu msingi, pamoja na kutopenda kuzaa na ukosefu wa usawa katika kazi n.k. Maelezo ya Papa , yametafakari kwa kina, tukio lililoandikwa katika Injili, Arusi ya Kana, ambako Yesu alifanya muujiza wake ya kwanza, kama mama yake Maria alivyoomba.

Papa anasema, katika Injili hii, Yesu anaonyesha upendo wake katika kuwajali wanandoa. Muujiza aliyoufanya katika arusi hii, ni  ishara yenye  mengi ya kutueleza juu ya maana na umuhimu wa ndoa yenyewe.  Papa alieleza na kuitazama jamii ya leo inayokabiliwa na mengi, wengi hawataki kufunga ndoa, na wengi kutaka kutangua ndoa zao, kuvunja ahadi waliyotoa mbele ya Mungu ya kuishi pamoja kama wanandoa. Na pia lengo la  kuzaa  watoto, siku hadi ziku linazidi kutupwa kapuni. 

Papa ameonya  kwamba , kuvunjika kwa kiungo msingi cha ahadi za ndoa , huathiri  vijana wengine kuiona ndoa kama vile ni jambo la  mpito au tukio la muda mfupi, linaloweza chezewa kimzaha. Papa amelitazama hilo kwa kina akisema pengine inatokana na  hali za wasiwasi na hofu zinazozuia  wanaume na wanawake, kujenga imani thabiti katika kutegemea neema nyingi za  ahadi za Kristo, katika ndoa na katika familia.

Lakini katika ukweli,  tunajua kwamba,  karibu kila mtu awe mwanamke au  mwanaume huwa na hamu kujenga mahusiano thabiti na ya kudumu katika uhusiano wake na mwenzake katika ndoa, na hufurahia  ndoa iliyo  imara na familia yenye furaha.Kuna shuhuda nyingi za wazi zenye  kuonyesha baraka za ndoa iliyo imara ya Kikristo, zenye maisha mazuri ya furaha na familia ya furaha. Papa alieleza na kutahadharisha kwamba, kwa kuweka wakfu upendo wao kwa Mungu,ahadi hiyo inakuwa ni chemichemi ya imani yao na uaminifu wao.  Na ili baraka hizi zionekane  dhahiri kwa  dunia, wanandoa wote wanapaswa kufurahia sawia matokeo ya upendo wao , yaani matunda mapya ya upendo wao ambao ni watoto,pamojana fursa sawa katika maisha y akila siku, iwe majumbani na sehemu za kazi; kuona  thamani mpya ya kuwa  mama au  baba; na katika kuona msaada wa thamani wanaotakiwa kuutoa kwa ajili ya familia hitaji..

Baba Mtakatifu ameeleza na kutoa mwaliko kwa wote kutokuwa na hofu ya kumwalika Yesu na Maria katika maisha yao ya ndoa. kwa kuwa ndoa ya Kikristo hufungwa si kwa manufaa ya maarusi wenyewe tu , lakini pia kwa manufaa ya jumuiya nzima na jamii kwa ujumla. Kwa sababu hiyo , inakuwa muhimu kama Wakristo , kudai haki sawa katika masuala yanayohusiana na ajira na ujira kwa kuwa ubaguzi huleta mtafaruko.  

Baada ya Katekesi hii  , Papa alisalimia mahujaji na wageni katika lugha mbalimbali , akiwaombea hija yao katika Mji Mkuu huu wa Imani , iweze kuwaimarisha katika upendo kwa Kristo na Kanisa lake. Kwao wote aliwapa baraka zake za Kipapa. Mungu awabariki wote!








All the contents on this site are copyrighted ©.