Waziri Mkuu wa Italia, Mateo Renzi , mapema Jumatano akizungumzia changamoto ya wahamiaji Ulaya, kabla ya kushiriki katika kikao cha Bunge la Ulaya kinachofanyika kesho Alhamisi, alitumaini Bunge la Ulaya litafanya majadiliano ya kina , yenye kutambua haja ya kutengeneza mkakati mbinu mpana zaidi wa kudumu , katika kukabiliana na wimbi la wahamiaji na wakimbizi ,badala ya kuwa na majibu ya mpito ya kurashia rashia harakaharaka, kama kuharibu vyombo vinavyotumika kusafirisha wahamiaji kinyume cha sheria.
Waziri Mkuu Renzi , alieleza hili akiwa katika ukumbi wa Bunge la Italia Montecitorio, ambamo alitaja umuhimu wa Wabunge kufikiria kwa kina zaidi, sababu msingi zinazozua wimbi hili jipya kubwa la uhamaji kwa nyakati hizi , kuliko ilivyokuwa miaka ya nyuma. Alisema hasa ni kujali nini kinaendelea Afrika. Bila kuanzia huko , majibu mengine yatakuwa ni majibu ya mpito ambayo hayatasaidia kusitisha ukatili unaoendelea kuangamiza maisha ya wana wa Afrika kwa wingi, wanaovuka bahari ya mediterrannea. Alieleza hili katika mtazamo makini kwamba, wakimbizi wanaopoteza maisha si tu kutoka Libya au Syria lakini kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika hasa ambako kuna matatizo ya njaa, vita na mgawanyiko wa Mabwana wa kisiasa.
Kwa hiyo akasema, mbele ya sura hii ya uhamiaji kutoka Afrika, Bunge la Italia
, kama inavyotakiwa pia kwa Bunge la Ulaya, wanawajibu wa kutengeneza mpango thabiti
wa miakamingi ijayo, kwa Italia na jukumu lake kama daraja la Ulaya na
Afrika. Na ametoa wito kwa mamlaka zote ya kisiasa, kutogawanyika katika utoaji
wa jibu thabiti linalofaa katika kukabiliana na changamoto hii. Na kwamba ni lazima
kutazama kwa makini asili ya kuenea kwa utamaduni wa ugaidi, kama wanataka kushinda
vita vinavyo angamiza wazo la dunia juu ya nguvukazi watu na juu ya utamaduni. Hivyo
jibu la kiufundi, kama ni nini kinazamisha boti, haliwezi kutatua mgogogro huu, bali
hasa ni kutatufa kwa nini watu wanahama katika nchi zao. Bunge la Jamhuri ya Italia
lina wajibu wa kutoa jibu lake katika hili.
Wakati huohuo , Mtandao wa Radio3 Mondo , umeandika, Mtandao wa uhalifu wa Italia maarufu kwa jina la Mafia, umebadilisha maeneo yake ya kazi kwa kuhamia Afrika , kama eneo lake jipya kwa shughuli zake. Leo hii Afrika,inathaminiwa sana na wapenda magendo nautajiri wa harakaharaka kutokana na utajiri wa maliasili zake. Afrika imekuwa ni siri msingi wa utendaji wa Mafia. Afrika kama chanzo kikuu cha migodi ya almasi, dhahabu, vilabu vya usiku na maeneo makubwa ya aridhi wanayojipatia kwa urahisi na uwezekano wa kumiliki miradi mingi kwa njia za rushwa na magendo. .
Radio3 Mondo, inasema , watu wenye mapenzi mema na Afrika ni muhimu kujiuliza ni njia zipi zinatumiwa na mfumo huo uliofichama wa Mafia kunufaika na utajiri wa Afrika ? Na iwapo jumuiya ya kimataifa kweli inafuatilia kwa nia makini kukomesha kuenea kwa mipango ya uchumi angamizi na matokeo yake mabovu kwa jamii Afrika. Redio hiyo imenukuu Chama cha Waandishi a Habari Vijana IIRPI, kwa kushirikiana na Mtandao wa Afrika wa Vituo kwa ajili ya Upelelezi ANCIR, ambao wameandika kwamba, Uchunguzi wa kimataifa unaoonyesha mtandao wa utendaji wa mafia kwa undani, umeingia katika mataifa 13 ya nchi za Afrika.
All the contents on this site are copyrighted ©. |