2015-04-22 09:11:00

Injili ya Uhai: Kifo laini si sehemu ya haki msingi za binadamu!


Baraza la Maaskofu Katoliki Colombia linapinga kitendo cha Serikali kuhalalisha kifo laini kwa njia ya sheria kwa kisingizio kwamba, hii ni haki msingi ya binadamu kwani inapingana kimsingi na uhai wa mwanadamu ambayo ni zawadi kubwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Wizara ya afya, kwa kuzingatia amri iliyotolewa na Mahakama kuu ya Rufa anchini humo tarehe 4 Machi 2015 imehalalisha kwamba, kifo laini, au Eutanasia ni haki msingi ya mgonjwa.

Baraza la Maaskofu katoliki Colombia linakazia kusema kwamba, kifo laini si sehemu ya haki msingi za binadamu na badala yake ni kosa kubwa dhidi ya utakatifu wa maisha ya binadamu, ambaye ameumbwa kwa sura na mfano wa Mungu. Wizara ya afya haiwezi kujichukulia mamlaka ya kuratibu masuala ya kifo laini, kwa vile tu kwamba, hakuna sheria inayozungumzia changamoto hii katika maisha ya wananchi wa Colombia.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.