Na Rais wa Italia , Sergio Matterella, akimtembelea Papa Francisko mjini Vatican mapema Jumamosi hii, katika hotuba yake, ameonyesha shukurani zake za dhati kwa Papa Francisco kwa ushuhuda wake wa thamani, wenye kuonyesha uhusiano maalum na wa kipekee kati ya Kiti Kitakatifu na Jamhuri ya Italia..Hivyo Rais Sergio, kwa niaba yake mwenyewe na kwa niaba ya Wananchi wa Italia ,alipenda kufikisha salaam za upendo, urafiki katika mahusiano haya yenye mwelekeo wa kukua siku baada ya siku.
Pia Rais ameshukuru kwa maneno ya matumaini yaliyotolewa Papa Francisko kwamba yatasaidia kuokoa thamani ya mshikamano na umoja wa watu wa Italia, katika mazingira ya nyakati hizi, zilizojaa wasiwasi na mashaka , kwenye wigo wa hisia za watu, hasa katika nyakati za mgogoro na shida. Na ameutaja uhusiano wa karibu kati ya Italia na Nchi ya Jiji la Vatican, kuwa umesimikwa katika mizizi na sura ya kipekee ya kihistoria, kama ujirani mwema kati ya mataifa haya mawili. Uhusiano unaoenezwa na kuendelezwa kwa njia ya kuheshimiana. Na pia alishukuru Mafundisho Papa, yenye kulenga moja kwa moja katika ukweli wote na hata juu ya masuala ya kijamii, kiuchumi na kisiasa ya Italia. Rais Mattarella alieleza na kurejea nyaraka mbalimbali za Kitume za Mapapa , zenye kuwa na utajiri wa maadili katikia kazi za kukuza, amani, maendeleo na , heshima ya binadamu.
Aidha Rais Matterella ,amerejea utendaji mbalimbali wa Papa Francisco, akitaja tangu ziara yake ya kwanza ya kichungaji nchini Italia katika eneo la Lampedusa, na ile aliyoifanyika hivi karibuni, Naples, ambamo katika zote alionyesha mshikamano wake katika kujali matatizo na matarajio ya Italia. Rais ameonyesha matumaini yake katika Jubilee ya Huruma ya Mungu aliyoitangaza Papa Francisko hivi karibuni kwamba, itatoa nafasi ya kutafakari juu ya thamani ya maadili ya haki na mshikamano wa kweli na maana ya kuwa na amani. Ameonyesha kutambua kwamba , katika wakati wetu huu mienendo ya kiuchumi mara nyingi inapoteza mwelekeo wa ubinadamu, na hivyo kujenga kitisho cha kuendeleza dhuluma, zenye kuishia katika migogoro na ukosefu wa usalama. Na hivyo wito wa kutafuta Huruma ya Mungu, unaweza kufufua upya miongoni mwa watu, maisha mapya yenye kuona thamani ya mahusiano mazuri ya kiuchumi na kijamii kwa ajili ya ustawi na maendeleo ya wote.
Na kwamba, Uhuru wa kidini ni ya matarajio halisi na msingi yaliyomo katika Katiba ya Italia. Ukiukaji wowote ule, inakuwa ni kuvunja haki za binadamu na jamii. Na hivyo vurugu zozote zinazofanywa dhidi ya jamii ya Kikristo katika baadhi ya maeneo, inakuwa ni changamoto dunia, inayohitaji kutafutiwa jibu la nguvu la pamoja katika dhamiri za wote wanaopenda uhuru na kuvumiliana. Italia anahisi nia, na mshikamano wa kimataifa kupambana na ugaidi , kuwa sehemu ya jumuiya ya kimataifa, kwa sababu ni utendaji wenye kuzingatia kanuni za maelewano na ushirikiano, sharti msingi kwa ajili ya amani ya kweli.
Rais Mattarella alikamilisha hotuba yake kwa kurudia kutoa upya mwaliko kwa Papa Francisko, aitembelee tena Ikulu ya Italia, kwa ajili ya kuimarisha zaidi mazungumzo yao, na kwa ajili ya mwendelezo wa mahusiano haya maalum yanayosindikiza uhusiano thabiti kati ya Kiti Kitakatifu na Jamhuri ya Italia.
All the contents on this site are copyrighted ©. |