2015-04-18 15:26:00

Siku ya Fray Junipero Serra: Papa Francisko kuadhimisha Ibada ya Misa


Baba Mtakatifu Francisko  anatarajiwa kutembelea na hatimaye kuadhimisha Ibada ya Misa Takatifu kwenye Chuo kikuu cha Wamarekani, Jumamosi tarehe 2 Mei 2015. Hayo yamethibitishwa na Padre Ciro Benedettin, Msemaji msaidizi wa Vatican alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari. Kabla ya tukio hili, Jumatatu tarehe 20 Aprili 2015 kutazinduliwa tafakari ya kina iliyoandaliwa na Tume ya Kipapa kwa ajili ya Amerika ya Kusini kwa kushirikiana na Chuo kikuu cha Kipapa cha Wamarekani, kilichoko mjini Roma.

Tafakari hii itaongozwa na tema “ Fra Junipero Serra, mtume wa Calfonia, shuhuda wa utakatifu wa maisha. Tafakari hii itatolewa na viongozi wakuu kutoka Tume ya Kipapa kwa ajili ya Amerika ya Kusini, Baraza la Kipapa linalowatangaza waamini kuwa wenyeheri na watakatifu pamoja na Gombera wa Chuo Kikuu cha Wamarekani, kilichoko mjini Roma.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.