2015-04-18 12:47:00

Papa atoa wito kwa Italia, kudumisha maadili yake ya Kikristo


Baba Mtakatifu Francisko mapema Jumamosi hii amekutana na Rais Sergio Mattarella wa Jamhuri ya Italia, ambamo wameweza kubadilishana mawazo juu ya mambo mbalimbali yanayogusa jamii ya Italia. Hii ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Papa kumpokea rasmi  mjini Vatican, Rais Sergio Mattarella, tangu  alipochaguliwa kuwa Rais wa Italia katika uchaguzi uliofanyika tarehe 3 Februari 2015.

Katika hotuba yake kwa Rais Sergio , Papa amesisitiza Italia kutosahau urithi wake wa Kikristo, katika shughuli zake zote za kimaendeleo na kisiasa na hasa kwa ajili ya udumishaji wa maelewano miongoni mwa raia wote wa Italia. Aidha Papa ametoa wito kwa Rais na taasisi zote za Italia, kusikiliza "kilio cha maumivu" ya vijana wengi ambao hawana kazi.  Papa pia alitumaini, maonyesho ya Kimataifa yanayofanyika  Milan “Expo 2015, itakuwa fursa nzuri ya kuchukua maamuzi yanayofaa kwa ajili ya utetezi wa mazingira.

Kukutana kwa viongozi hawa, Papa Francisko  na Rais Mattarella, kunatajwa kuwa   ishara thabiti ya  maelewano  kati ya watu wa Italia na Jimbo Takatifu,  kama Papa alivyobaini, inarejesha upya  neema hii ya ushirikiano wa tangu maamuzi yaliyotenganisha  majukumu na wajibikaji kati ya serikali ya Italia na  Serikali ya Jiji la Vatican, kama jambo muhimu, lililoonyesha  uwepo wa haja ya kutengeneza mfumo mpya wa ushirikiano,  kwa ajili ya mema  ya kawaida kwa watu wa Italia na serikali ya Jimbo la Papa.  Papa kwa  upande mwingine, alibainisha, Kanisa linahitaji hali  utulivu na amani miongozni mwa jamii kwa ajili ya kutekeleza utume wake wa kiroho. Hali inayoweza kufanikishwa na kukuzwa na mamlaka ya umma.  Na kwamba,  maendeleo ya jamii yenye wingi wa mchanganyiko wa watu mbalimbali, haiwezi kudai kutoona  hali halisi zenye kusukuma  umuhimu wa uwepo wa  maendeleo ya kidini ya kweli,  si tu yenye kulishwa na urafiki,  lakini katika kutambua  wajibu wake katika ujenzi wa jamii tulivu,nyenye mshikamano na umoja..

Papa ameonyesha imani yake kwa Rais Mattarella, aliyekua ndani ya malezi ya Kikristo, kwamba, ataweza kutoa mchango mkubwa katika kukuza mwendelezo wa  utamaduni wa Kikristo, msingi wa historia ya Italia na tabia ya watu wa Italia.  Imani yenye kuwa utendaji wa kazi wa kila siku kwa  taasisi zake, zikionyesha sura na historia ya pekee na uwajibikaji katika  nyanja zote za maisha ya Waitaliano, tangu ndani ya familia shule ya kwanza ya mshikamano na shule maadili, ambavyo husaidia kuijumuisha jamii katika utendaji wake kama sehemu ya malezi msingi ya mtu.

Aidha Papa Francisko alitoa ombi kwa Rais Mattarella, kusikiliza  kwa makini kilio cha uchungu cha vijana wasiokuwa na ajira, akisema kati ya mazuri yote  ya kimaendeleo, ni  muhimu  juhudi zote za pamoja , kutambua  kazi, katika umashuhuri wake wa kujenga uhusiano wenye kuwa na  utu sawa, na uwezekano wa kujenga maisha yenye heshima na uhuru. Katika kukabiliana na changamoto hii, Papa anasema jumuiya ya kanisa, itafanya kazi bega kwa bega, katika kupata ufumbuzi wa tatizo hili, kuwa kipaumbele katika utafutaji wa haki. Kwa namna ya kipekee vijana wanahitaji kufanya kazi , ili waweze kuwa na maisha ya utulivu, na hivyo kuondokana na vishawishi vya kuingia katika utendaji usiofaa na majaribu yenye kuhatarisha usalama .

Aidha Papa katika hotuba yake , hakusahau kutoa shukurani zake kwa serikali ya Italia kwa juhudi inazofanya katika kuwapokea mamia ya wageni wahamiaji  na wakimbizi wanaotafuta kusalimisha maisha yao. Papa amesema hii ni hazina kubwa kwa Italia katika kudumisha mila na utamaduni i wake, wenye kulishwa na kuvuviwa na imani ya Kikristo, kwa ajili ya kufanikisha maendeleo na  maelewano, kama mchango wake katika sadaka ya kujenga amani na haki duniani. 








All the contents on this site are copyrighted ©.