2015-04-15 10:07:00

Ukweli utawaweka huru!


Kumbu kumbu ya maadhimisho ya miaka mia moja tangu mauaji ya Waarmeni yalipotokea, iliadhimishwa na Baba Mtakatifu Francisko kwenye Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican, Jumapili ya huruma ya Mungu, hapo tarehe 12 Aprili 2015. Baba Mtakatifu mwanzoni mwa Ibada hii alinukuu maneno yaliyomo kwenye tamko la pamoja lililotiwa sahihi kati ya Papa Yohane Paulo II na Patriaki Karekin II kunako mwaka 2001, waliozungumzia mauaji ya kimbari dhidi ya Waarmeni yaliyofanyika kuanzia mwaka 1915;  mauaji ambayo kwa wengi yanajulikana kama “mauaji ya kwanza ya kimbari katika Karne ya 21”.

Baba Mtakatifu katika salam zake, alionesha matumaini kwamba, wananchi wa Uturuki na Armenia kwa pamoja wataanza hija ya upatanisho. Maneno haya ya Baba Mtakatifu Francisko “yametibua” nyongo ya Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki kwa kutoa maneno makali dhidi ya Baba Mtakatifu. Lakini, wakati huo huo, amewataka wananchi wa Armenia kuunda tume ya pamoja na Uturuki, ili kuchunguza matukio haya ya kihistoria kati ya nchi hizi mbili, ili kubainisha ukweli wa mambo!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.