Tunasikitika kutangaza kifo cha Kardinali Roberto Tucci, kilichotokea siku ya Jumanne usiku mjini Roma, ikiwa zimebaki siku chache kutimiza miaka 94 ya kuzaliwa hapo tarehe 19 Aprili. Kardinali Tucci alijiunga na Wajesuit na kupata daraja la Upadre mwaka 1950, na baadaye alijipatia shahada ya uzamili katika masomo ya kitaalimungu katika Chuo Kikuu cha Kipapa Gregorian kilichoko mjini Roma
Pamoja na huduma za kikuhani, pia alifundisha kwa miaka kadhaa katika Kitivo Teolojia
katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Louis cha Naples, pia akiwa Mkurugenzi wa jarida
la Wajesuit la Civilta Catolica kati ya mwaka 1959-1973. Na baadaye akateuliwa kuwa
Mkurugenzi Mkuu wa Redio Vatican, utume alioutumikia kati ya 1973-1985. Alifanywa
Kardinali na Papa Yohana Paul II mnamo Februari 21, 2001. Kati ya majukumu mengine
, aliwahi pia kuwa mratibu wa safari za Papa Yohana Paul II. .
Aidha Marehemu Kardinali Tucci, anakumbukwa kwa kazi kubwa aliyoifanya wakati wa Mkutano
Mkuu wa Pili wa Vatican ,ambamo alishiriki kazi za kuandaa nyaraka za majadiliano
ya Baraza, na vikao mbalimbali kama mtalaam wa teolojia. Pia alitoa mchango mkubwa
katika toleo la mwisho la Katiba ya Kichungaji “Gaudium et Spes”
Taarifa imetolewa kwamba, Jumatano 15 Aprili, majira ya saa sita, katika Jengo la Makao Makuu ya Wajesuit hapa Roma, Mtaa wa Borgo San Spirito Namba 4, Mwili wa Marehemu utaweka katika chumba maalu , kwa ajili ya kutoa heshima za Mwisho kwa Marehemu. Siku ya Ijumaa 17 Aprili majira ya saa saba na nusu za mchana , Mwili wa Marehemu utahamia katika Altare ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, kwa ajili ya Ibada ya Misa ya wafu na Maziko, itakayoongozwa na Kardinali Angelo Sodano , Mkuu wa Dekania ya Makardinali, majira ya saa kumi na nusu za jioni. Papa Francisko , ataongoza Ibada ya mazishi. Tunaiombea Roho yake pumziko la amani.
All the contents on this site are copyrighted ©. |