2015-04-13 12:06:00

Mons. Paolo R. Gualtieri ateuliwa kuwa Balozi wa Vatican Madagascar


Baba Mtakatifu Francisko amemteua Monsinyo Paolo Rocco Gualtieri kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Madagascar na kumpandisha hadhi kuwa Askofu mkuu. Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu mteule Gualtieri alizaliwa huko Supersano, Lecce, Italia kunako tareh 1 Februari 1961. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, akapadrishwa kunako tarehe 24 Septemba 1988.

Amejiendeleza kimasomo na kujipatia shahada ya uzamivu pamoja na shahada ya uzamili katika mafundisho tanzu ya Kanisa. Alianza utume wake wa kidiplomasia mjini Vatican kunako tarehe 1 Julai 1996. Tangu wakati huo, amefanya kazi nchini Papua New Guinea, Jamhuri ya Wananchi wa Dominikan pamoja na idara ya mambo ya nchi za nje na uhusiano wa kimataifa mjini Vatican.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.