2015-04-08 15:28:00

Mauaji ya Rwanda yakumbukwa


Miaka 21 baada ya mauaji ya kimbari Rwanda –kutosahau na  kusamehe .
Jumanne  ilitimia miaka 21, tangu yalipofanyika mauaji ya kimbali nchini Rwanda. Ilikuwa ni tarehe 7 Aprili 1994, wakati Rwanda ilipoanza kushuhudia mwanzo wa siku mia za sadaka ya watu kuteketezwa kwa watu  karibia milioni moja kwa  ghadhabu isiyo na kipimo ya Wahutu dhidi ya  Watutsi, wengi wao ikiwa kwa kukatwa kwa mapanga. Hasira zinazotajwa kuchochewa na ulipizaji  kisasi kwa mauaji ya  Rais Juvenal Habyarimana, ambaye alikufa siku moja kabla, Aprili 6, kwa ndege aliyokuwa akisafiria kurushiwa kombora wakati  akirejea nchini mwake tokea ziara ya kikazi.  Mpaka sasa mtu aliyehusika na  mauaji bado hajulikani lakini mauaji ni mauaji yaliyo fungua moja ya kurasa nzito katika  historia ya Afrika, sanjari na kutojali kwa jumla kwa  jumuiya ya kimataifa.

Hadi leo hii, pamoja na kupita kwa miaka 21 , bado mioyo ya watu wengi wa Rwanda , wanaishi katika hali za majonzi , ingawa Jumuiya ya Kimataifa ilianzisha juhudi za kuwaleta mbele ya sheria wahalifu , kwa kuanzisha Mahakama ya Uhalifu wa kivita mjini  Arusha, Tanzania, hasa kufuatilia Mauaji ya Kimbari ya Rwanda.  Umoja wa Mataifa pamoja na Ujumbe wa Kudumu wa Rwanda kwenye Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kumbukumbu hii, waliandaa tumbuizo maalum jijini New York, kukumbuka mateso dhidi ya watutsi na baadhi ya wahutu walioyoyapitia nchini Rwanda mwaka 1994. Khafla iliyohudhuriwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, na  Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na watu wenigne mashuhuri duniani.

Katika kumbukumbu hii, jumuiya ya kimataifa imemhimiza Katibu Mkuu wa Umoja wa kuchukua hatua kwa madhubuti na kwa wakati muafaka kuzuia mauaji dhidi ya binadamu. Nae  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon, katika  ujumbe wake, kwa ajili hiyo, amesema ni muhimu kwa ajili ya matengenezo ya amani na usalama kutenda kabla ya hali haijazorota. Na kwamba,  maadhimisho ya kila mwaka ya Siku ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari yanayo fanya rejea katika mauaji ya Rwanda, kwa mwaka huu yamekuwa na  maana zaidi, kutokana na  mwaka huu kuadhimisha  miaka 70 ya kuanzishwa kwa  Umoja wa Mataifa.

Katika ujumbe wake, Ban Ki-moon amesema Siku ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda inakuwa ni wakati wa kumbukumbu kwa heshima ya  watu zaidi ya 800,000 waliouawa katika kipindi cha miezi mitatu nchini  Rwanda . Wengi wa waathirika wakiwa Watutsi,i pia ni pamoja na  Wahutu, Watwa na wengine, wasiokuwa na ubabe wa kupindukia kisiasa.
Ban Ki-moon ametoa  wito kwa kutumia maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa kuangalia siku za nyuma,  na kufanya majumuisho katika  kukabiliana na changamoto za sasa na maamuzi mapya ya pamoja kwa ajili ya  kuzuia mauaji kama hayo kutokea tena.

Amelaani migogoro na mauaji katika sehemu nyingi za dunia kwamba  huendelea kugawanya jamii, kuua na watu kuhama  maeneo yao,  hali inayo dhoofisha uchumi na kuharibu urithi wa utamaduni.

Ban ameeleza na kuonyesha kujali kwamba , nchi nyingi sasa zinakabiliwa na hatari za kuvuruga  usalama wa wananchi , na hivyo wengi  kukabiliwa na ukatili wa migogoro yenye vurugu hasa kwa makundi ya watu maskini. Na kwamba, ubaguzi huendelea kusambaratisha jamii kivita, na  kuua demokrasia msingi wa amani na furaha katika jamii. 








All the contents on this site are copyrighted ©.