Homilia ya Baba Mtakatifu Francisko kwa wakati wa Mkesha wa Papa, ilianza na tafakari juu ya tukio lenyewe akisema , katika usiku huu wa mkesha, Bwana hatasinzia wala hatalala, ni mlinzi kwa watu wake, hadi atakapowatoa katika utumwa , akiiweka wazi mbele yao njia ya uhuru. Papa aliongoza Ibada ya Mkesha wa Pasaka , katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, Usiku wa Jumamosi Kuu.
Papa aliuzungumzia Usiku huu Mkuu , ambamo Bwana anakesha na kwa nguvu ya upendo
wake , anawapitisha watu wake katika Bahari ya Shamu, na ndivyo anavyomleta Yesu kupitia
njia ya dimbwi la kifo na dunia ya kuzimu.
Huu ulikuwa ni usiku wa mkesha kwa wanafunzi wa Yesu, usiku wa uchungu na hofu kuu.
Wanaume walibaki wamejifungia katika chumba cha Juu . Lakini wanawake alfajiri ya
baada ya Sabato, walienda kaburini, kwa nia ya kutaka kuupaka mafuta mwili wa Yesu.
Mioyo yao ilijaa mashaka , wakijiuliza maswali mengi, watawezaje kuingia ndani , nani
atakaye waondolea lile jiwe la mlangoni pa kaburi? ... Lakini mara walipata ishara
ya kwanza ya kuingia ndani, jiwe kubwa walilokuwa wakilihofia , lilikuwa tayari
limeviringishwa mbali na kaburi hilo. Kaburi lilikuwa wazi!
Na walipoingia kaburini walimwona kijana ameketi upande wa kulia, aliyevaa vazi jeupe
..." (Mk 16.5). Hivyo wanawake walikuwa wa kwanza kuona ishara hii kubwa: kaburi tupu,
na walikuwa wa kwanza kuingia ...
Baba Mtakatifu alifafanua kiliturujia maana ya kuingia ndani ya kaburi, akisema
kuwa ni jambo jema wakati wa Mkesha huu, kupata uzoefu wa wanawake hao . Na hiyo
ndiyo ilikuwa maana ya kushiriki kaika Ibada ya Mkesha wa Pasaka. Maana yake ni
kuingia ndani ya fumbo, ambamo Mungu anakamilisha kazi yake ulinzi kwa upendo. Na
hatuwezi kuwa na Pasaka bila ya kuingia katika fumbo hili. Si kwa ujanja wa akili,
au jambo tunalolifahamu au kulisoma habari zake , lakini ni zaidi ya hayo, ni mengi
zaidi!
Na kwamba , kuingia katika fumbo hili, maana yake ni kuwa na uwezo wa kuona maajabu
haya , ni kuwa na uwezo wa kusikiliza ukimya na ming’ong’no midogo kati ya ukimya
ambamo Mungu anazungumza nasi (cf. 1 Wafalme 19:12).
Kuingia katika fumbo hili , kunatutaka kutohofia hali halisi. Ina maana tusibaki
tumejifungia katika dhambi zetu na mambo tuliyozoea , tusijifungie ndani mwetu ,
na wala si kuyakimbia yale tusiyoyaelewa , na si kufumbia macho matatizo ya wengine
au kukanusha au kuyafuta maswali ... Bali kuingia katika fumbo huili ina maana ya
kuyashiriki pia matatizo ya wenzetu , tukijikatalia hali nzuri za maisha yetu ,ni
kuuweka uzembe na tofauti zinazoturudisha nyuma , katika mwendo ni kusonga mbele
kuutafuta ukweli, uzuri na upendo wa Mungu. Ni kutafuta maana ya kina ya jibu, ambalo
si la kijuujuu katika hoja zinazokuwa changamoto kwa imani yetu, uaminifu wetu na
uhalisi wetu.
Kuingia katika fumbo hili, tunahitaji unyenyekevu, kuushusha ufahari wetu binafsi,
kushuka toka kinara cha mimi na dhania zetu , na kuwa na unyenyekevu wa kutojiona
wa maana kuliko wengine, ni kutambua hadhi yetu kwamba , ni viumbe wenye dhaifu,
wenye dhambi wanaohitaji msamaha. Kuingia katika fumbo hili inahitaji kujishusha
kijasiri , katika kukataa uovu tunayopenda kuabudu. .
Papa Francisco aliendelea kusema, Wanawake wa kwanza, wafuasi wa Yesu wanatufundisha
sisi yote hayo. Katika Usiku wa Jumamosi Kuu , waliukesha usiku ule wakiwa na Maria.
Na Bikira Maria aliwasaidia kutopoteza imani na tumaini. Kama matokeo yake , hawakubaki
kama wafungwa wa hofu na huzuni ,maana mara mwanga wa siku ulivyotokea , walichukua
mikononi mwao, marhamu, mioyo yao ikiwa imepakwa mafuta ya upendo. Walikwenda na
kukuta kaburi li wazi na kuingia ndani ya fumbo la Pasaka. Hili linatufundisha sisi
kukesha na Mungu, tukiwa karibu na Mama yetu Maria , ili pia sisi tuweze kuingia katika
fumbo hili la kutoka katika kifo hadi maisha.
All the contents on this site are copyrighted ©. |