2015-03-29 10:54:00

Vijana kutoka Afrika Mashariki wamefunika, Kanisa kuu la Mt. Petro!


Wakati wa sala ya waamini, kwenye Ibada ya Misa Takatifu, Jumapili ya Matawi, mwanzo wa Juma kuu la mateso, kifo na ufufuko wa Kristo, waamini kwenye Uwanja wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican wamesali ili kwamba, mateso ya Yesu aliyoyapokea hadi kufa Msalabani, yawawezeshe waamini kujitosa bila ya kujibakiza ili kutangaza Injili ya Kristo.

Waamini wajifunze kukubali na kupokea mateso ya Yesu kwa uhuru kama sehemu ya mchakato wa kushiriki katika kazi ya ukombozi. Mateso ya Yesu Kristo kielelezo cha utii na utekelezaji wa mapenzi ya Baba yake wa mbinguni, yawasaidie waamini kuwa wakarimu, wenye mioyo safi na isiyogawanyika. Waamini wanakumbushwa kwamba, Yesu ameteseka kwa ajili ya kumkomboa mwanadamu, awafariji katika madonda yao na kuwawashia tena matumaini. Hii ni sala kwa lugha ya Kiswahili iliyosomwa na Sr. Stella Felix Kimaro, kutoka Tanzania.

Maadhimisho ya Siku ya 30 ya Vijana Kimataifa, yatakumbukwa sana na Shemasi Aristid Shayo na Justus Okibo ambao wamekuwa karibu sana na Baba Mtakatifu Francisko wakati wa maadhimisho ya Ibada ya Misa Takatifu, kama wahudumu wa Altare ya Bwana.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.