2015-03-25 10:59:00

Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania: Familia na Mwaka wa Watawa!


Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican inaendelea kukushirikisha Ujumbe wa Kwaresima kutoka kwa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania unaoongozwa na kauli mbiu “Zingatieni haki na kutenda mema. Sura ya kwanza, tulikushirikisha kuhusu haki, sura ya pili tukajadili kuhusu haki na tunu zake; matendo mema kama ushuhuda wa imani. Leo tunaingia katika sura ya tatu: Sinodi ya Familia na Mwaka wa Watawa Duniani.

SURA YA TATU

MATUKIO YA KIKANISA

Sinodi ya Familia

12. Tukiwa bado tunakumbukumbu hai ya Sinodi ya Familia iliyofanyika mwishoni mwa mwaka jana huko Roma,tunapata nafasi ya kuendelea kutafakari na kujifunza juu ya chimbuko, asili na malengo ya familia kadiri ya mpango wa Mungu. Tunatambua kuwa familia hupata utambulisho na dhima yake katika mpango wa Mungu wauumbaji na ukombozi ikielekezwa juu ya kile inachowezakufanya na inachopaswa kutenda.3 Kila familia inapaswakutambua ndani mwake wito wake ambao hauwezi kupuuzwa, na ambao ni heshima na haki yake na wajibu wake mkuu. Tunapaswa kukumbuka daima kuwa, “mustakabali wa Kanisa na ubinadamu unazaliwa na kukua katika familia”. Kwa uelewa huo tunazialika familia kurudi daima kwenye lengo la mwanzo na la asili ya familia kama lilivyoratibiwa na Mungu. Hii ni fursa yakujifahamu na ya kuufahamu wito na utume wa familiaambao unapaswa kuwa dira ya kuongoza safari ya familia za kikristo zilizo msingi wa Kanisa lililo Familia hasa yaMungu.

13. Katika mpango wa Mungu familia ni jumuiya mwandani ya uhai na upendo ikiwa na dhima ya kudumisha uhai na upendo hadi kuufikia ukamilifu wake kama wote walioumbwa na kukombolewa wanavyotakiwakujitahidi. Familia ndiyo “hekalu la uhai wa binadamu”  na chembe hai ya jamii, Kanisa na nchi yetu. Katika familia, baba, mama na watoto hujifunza mambo yote ya msingi kama kuheshimiana, kupendana, kusaidiana nakuwajibikiana. Humo wote hubaini pia sura ya Mungu na iwapo mafunzo yote hayo yanakosekana, jamii nzimahuteseka kwa ukatili huo na huwa chimbuko la ziada yaukatili. Kila mfumo wa jamii unawajibu wa kuhakikisha familia zinawezeshwa kuendelea kuwa muhimili wa maisha bora na endelevu kiuchumi na kimaadili. Hata hivyo, jamii inawajibu wa kutambua kuwa familia ina haki zake ambazo hakuna anayeweza kuinyang’anya kwani zimetoka kwa Mungu mwenyewe. Ni katikafamilia mtoto anaweza kupata haki zake zote za mwilina roho na uhai wake kulindwa. Familia kama taasisi ya msingi kabisa inapaswa kulindwa ikianzia kulinda uhai wa wanafamilia toka kutungwa mimba mpaka kifo cha kawaida. Pasipo familia taifa halitakuwepo!

Hata hivyo, familia zinapita katika kipindi kigumusana. Katika familia, ndiko tunakokuta manyanyaso na dhuluma kubwa wanazofanyiana wanafamilia pasipo udhibiti wowote. Utamaduni wa uonevu haswakwa watoto na wanawake unajenga tabia za ukatili nauhalifu sugu katika familia kama taasisi asilia. Katika mazingira haya ni lazima tusimame na kuitetea taasisi ya familia kama ilivyoratibiwa katika mpango wa Mungu.Familia hujenga jumuiya ya watu, huhudumia uhai wawanajumuia na kupokea uhai mpya; ni mshirika mkuu wa kwanza wa maendeleo na ustawi wa jamii na mhusika mkuu katika dhima za Serikali na Kanisa. Kwa hiyo ni wajibu wa kila mmoja kuilinda familia. Mwaka huu pia, Kanisa litaendelea kutafakari nafasi na dhima ya familia katika Sinodi ya Kawaida ya Maaskofu itakayofanyikaRoma mwezi Oktoba 2015. Huu ni mwaliko wa kuzidi kujizamisha katika tafakari na mikakati ya kujenga na kulinda familia zetu ili nazo ziilinde na kuijenga jamii.

Mwaka wa Watawa Duniani

14. Baba Mtakatifu Fransisko ameutangaza mwaka huu Novemba 2014 – Februari 2016 kuwa Mwaka wa Watawa. Sisi Kanisa la Tanzania tumeupokea mwaliko huu kwa moyo wa shukrani tukitambua mchango mkubwa wa watawa katika utume wa Kanisa. Wapendwa watawa “twamshukuru Mungu sikuzote kwa ajili yenu nyote… Wala hatuachi kuikumbuka kazi yenu ya imani, na taabu yenu ya upendo, na saburi yenu ya tumaini lililo katika Bwana wetu Yesu Kristo” (1 Thes 1: 1-5). Katika mwaka huu tungependa kuwahimiza watawa kurudi katika roho ya karama ya mashirika yenu. Litakuwa jambo la hatarikubwa kama shirika la kitawa litapoteza njia na kuiacharoho ya karama ya shirika. Mwaka huu uwe wa tafakari kwenu na kipindi cha kurudi daima kwenye chemchemi za maisha ya kikristo na za roho ya mwanzoni ya mashirika yenu.

Tunapenda pia kuwahimiza mfanye bidii katika utume wenu ili mlipambe Kanisa, nalo limdhihirishe Kristo,“kwa waamini na wasioamini”, huku mkimpeleka na kumfikisha Kristo kwa watu.

15. Watawa kimsingi wanafanya kazi katika Kanisa mahalia. Uhusiano wa mashirika na uongozi wa majimbo naounapaswa uzidi kuboreshwa, ili huduma na utume wa Kanisa uzidi kuimarika. Utambuzi na umuhimu wa mashirika ya kitawa kutenda shughuli ndani ya jimboyakiwa yameunganika na uongozi wa Kanisa mahali ni wa kuzingatia sana.

16. Mwaka huu pia unapaswa kuwa fursa ya kutathiminina kuona ni kwa jinsi gani miito ya utawa inavyokua. Ni vema kuendelea kuhimiza miito. Namna ya kwanzaya kuhimiza miito iwe ni kwa mfano wa maisha yetu.Maisha ya kielelezo na ya kujitoa ni ya muhimu na hiindio namna bora ya kuufanya wito wa utawa uchanue nakupendwa. Vijana wakivutiwa kuingia utawa kwa sababu nyingine yoyote zaidi ya kumfanya Kristo apendwe naKanisa liendelee kutimiza wito wake, basi lengo lote la maisha ya utawa litapotea.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican itaendelea kukuletea sehemu ya nne: wajibu wa Kijamii wa Kanisa! Usikose kujiunga nasi pamoja na kuwashirikisha jirani zako!

 








All the contents on this site are copyrighted ©.