2015-03-23 15:19:00

Siku ya furaha kimataifa!


Kwa azimio la Baraza la Umoja wa Mataifa namba 66/281, la Julai 12, 2012, tarehe 20 Machi ya kila mwaka, Jumuiya ya Kimataifa inaadhimisha Siku ya furaha duniani, haki msingi kwa kila bindamu. Ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon, umesisitiza kwamba, dunia inahitaji kuwa na mipango yenye uwiano mzuri katika nguzo tatu kuu za maendeleo: jamii, uchumi na mazingira kama mambo yasiyotengana. Na kwamba, kwa pamoja huweza kutoa maana pana katika uwepo wa  furaha duniani. 

Umoja wa Mataifa  umetoa mwaliko kwa nchi  wanachama, Mashirika ya Kimataifa na kimkoa, na pia vyama vya kiraia , yakiwemo mashirika yasiyokuwa ya kiserikali  na watu binafsi, kuwa na mipango ya kufanikisha  furaha kwa watu wake, hasa kupitia njia ya elimu na shughuli zinazoweza kuhamasisha  jamii kuwa na maisha ya furaha.

 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anasema "Furaha kwa familia  nzima ya binadamu ni moja ya malengo makuu ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kudumisha amani,  mafanikio, na maisha na utu kwa wote" . "Umoja wa Mataifa unataka  watu wote, wanawake na watoto kufurahia haki zao zote za binadamu; unataka  nchi zote kujua hadhi ya amani, na unapenda watu wote duniani  wabarikiwe sawa katika uwepo wa maendeleo endelevu, na hasa kwa wale wanaoachwa nyuma kutoka na  athari za janga la mabadiliko ya hali ya hewa".

 

 

Kama sehemu ya juhudi zake za Umoja wa Mataifa  kwa kushirikiana na wasanii wa kimataifa katika uwanja wa muziki, katika kusisitiza umuhimu wa furaha katika maisha ya kila siku, umezindua kampeni na ombi kwa raia wa dunia, kupitia “mtandano wa  "Streaming MixRadio" kuteua wimbo au muziki unaoweza kuleta  tabasamu kwa kila mtu.  Kampeni hii inalenga kuhamasisha matumaini bora kwa ajili ya  kesho .

 

Taarifa inasema,  Ban aliteua wimbo wenye ujumbe wa amani  wa  Stevie Wonder , ambao kwake, unasikika  kama sauti za furaha katika uwepo wa makubaliano mapya juu ya malengo ya maendeleo endelevu, katika yote ajenda za viongozi wa kimataifa zitakazojadiliwa baadaye mwaka huu .

 

Kundi la Mawakili mashuhuri akiwemo  Charlize Theron, Lang Lang, Michael Douglas, Angelique Kidjo, pamoja na wasanii wa kimataifa kama vile James Blunt, Idris Elba, David Guetta, John Legend, Cody Simpson na Pharrell Williams, pia wamechangia maoni yao katika kutunga wimbo maalum juu ya kujenga dunia yenye furaha, uliozinduliwa tarehe 20 Machi, 2015.

 

Bwana Ban Ki moon akitoa shukrani zake za dhati kwa wasanii hao, pia alitoa wito kwa watu wote , wawe na juhudi binafsi kwa ajili ya kudumisha furaha duniani.








All the contents on this site are copyrighted ©.