2015-03-19 15:15:00

Mashambulizi ya kigaidi yanatikisa utakatifu wa maisha


Baba Mtakatifu Francisko ametuma salam za rambi rambi kwa Askofu mkuu Ilario Antoniazzi wa Jimbo kuu la Tunisi, nchini Tunisia, kufuatia shambulizi la kigaidi lililosababisha watu 23 kufariki dunia na wengine kadhaa kujeruhiwa vibaya, Jumatano tarehe 18 Machi 2015.

 

Katika ujumbe ulioandikwa kwa niaba ya Baba Mtakatifu na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican, Baba Mtakatifu anashutumu vikali mashambulizi dhidi ya misingi ya haki na amani sanjari na utakatifu wa maisha ya mwanadamu. Baba Mtakatifu anaungana na ndugu, jamaa na wote walioguswa na janga hili na kwa namna ya pekee na Familia ya Mungu nchini Tunisia. Baba Mtakatifu anawaombea pumziko la milele wale wote waliofariki dunia; na wagonjwa waweze kupona na kurejea tena katika shughuli zao za kawaida.

 

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.