2015-03-16 14:30:00

San Marino na vatican kushirikiana zaidi


Baba Mtakatifu Francisko, Jumatatu tarehe 16 Machi 2015 amekutana na kuzungumza na Makapteni Giancarlo Terenzi na Guerrino Zanotti kutoka Jamhuri ya Watu wa San Marino waliomtembelea mjini Vatican. Baadaye Makapteni hawa wamekutana na kuzungumza na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican aliyekuwa ameambatana na Askofu mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu mkuu wa Mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa mjini Vatican.

 

Viongozi hawa katika mazungumzo yao, wameridhishwa na mahusiano mema yaliyopo kati ya nchi hizi mbili na kwa namna ya pekee, mchango unaotolewa na taasisi za Kanisa katika ustawi na maendeleo ya wananchi wa Jamhuri ya San Marino. Ni matumaini ya viongozi hawa kwamba,  nchi hizi mbili zitaendelea kushirikiana katika masuala ya kimataifa.

 

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican








All the contents on this site are copyrighted ©.