Bara la Afrika limeonywa dhidi ya kuiga kipofu, majawabu ya mabara mengine katika
kutatua matatizo ya Afrika. Onyo hilo, limetolewa na watafiti wa Kimataifa wa Taasisi
ya Sera ya Chakula na Utafiti, IFPRI.
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari
inasema, nchi za Kiafrika zisiige kiholela au kupitisha mikakati ya sera ya chakula
kipofu, katika lengo lake la kufanikisha mapinduzi ya kijani. NI lazima mikakati
ya utekelezaji ilenge katika hali halisi za matatizo mahalia ya Afrika. IFPRI, imetoa
ushauri huo, kwa kuzingatia matokea ya utafiti wake uliofanyika nchini Ghana.
Matokeo
ya awali yaliyochapishwa katika jarida Sera ya Chakula, yalionyesha kwamba, Afrika
badala ya kulenga tu katika uzalishaji wa chakula, ni lazima kuwa na mbadala wa kuendeleza
teknolojia mpya, katika kuboresha pia pato la miti na mazao ya mizizi, ambayo hupatikana
kwa wingi katika kanda ya Afrika, na pia kama njia ya kupunguza uzito wa kazi za
mikono kwa wananchi wa Afrika.
Matokeo ya utafiti huo yameanisha, Mapinduzi
ya Kijani ya miaka ya 1960 na 1970, katika nchi za Asia na Amerika ya Kusini, zilizo
weza kufanikisha ongezeko kubwa katika uzalishaji wa ngano na mazao mengine ya chakula,
kwa kutumia mbinu mpya za kilimo na hasa zaidi kuongeza matumizi ya mbolea na kilimo
cha umwagiliaji. Nchi za Afrika pamoja na kuwa na hamu ya kuiga mafanikio hayo, na
kupitishwa sera zinazofanana, hazijafanikiwa kuongeza mazao ya kilimo.
Mtafiti
Mkuu wa IFPRI, Alejandro Nin-Pratt, katika taarifa hiyo anaonya Afrika, isifanye kosa
jingine la kuiga kiholela mtindo uliofanikisha kuleta mapinduzi kijani barani Asia
, na hivyo kuepuka kukatishwa tamaa iwapo malengo yatashindwa kufanikiwa kama inavyotazamiwa
kufikia ukuaji endelevu katika kilimo.
Hapo Februari 19, Nin-Pratt alipokea
tuzo ya Elsevier Atlas, kwa kazi yake ya kina, katika kuona sababu zinazoweza kufanikisha
muafaka kwa Mapinduzi ya Kijani kwa nchi za Afrika. Tuzo Atlas hutoa hutolewa kama
kuheshimu kazi kubwa iliyofanywa na watafiti katika kutoa mchango mkubwa katika kufanikisha
maendeleo ya binadamu kwa njia ya sayansi.
Utafiti wa Nin-Pratt, ulilenga
kwa wakulima wadogowadogo nchini Ghana, ambao hutumia mbolea kidogo, wakichukuliwa
kama mfano kwa mataifa mengine ya Afrika . Ghana ilichaguliwa kwa ajili ya utafiti
kutokana na uwezo wake katika ukuaji wa haraka wa idadi ya watu na utendaji a kuonekana
katika mabadiliko ya kilimo. Imeonekana kasi ya ongezeko la watu Afrika, haina matokeo
ya kupunguza gharama za nguvu kazi katika kazi za kilimo.