2015-02-21 16:55:25

Askofu mkuu Edgar Pena Parra ateuliwa kuwa Balozi wa Vatican nchini Msumbiji


Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu mkuu Edgar Pena Parra, kuwa Balozi Mpya wa Vatican nchini Msumbiji. Hadi kuteuliwa kwake, alikuwa ni Balozi wa Vatican nchini Pakistan.

Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu Edgar Pena Parra, alizaliwa kunako tarehe 3 Machi 1960, nchini Venezuela. Baada ya masomo na majiundo yake ya kikasisi, akapadrishwa kunako tarehe 23 Agosti 1985. Tarehe 1 Aprili 1993 akaanza utume wake wa Kidiplomasia mjini Vatican. Tarehe 8 Januari 2011 akateuliwa na Baba Mtakatifu mstaafu Benedikto XVI kuwa Askofu mkuu na kuwekwa wakfu hapo tarehe 5 februari 2011 kwenye Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.







All the contents on this site are copyrighted ©.