Hivi karibuni, Jimbo kuu la Tabora, Tanzania liliadhimisha Sinodi ya Jimbo iliyokuwa
inaongozwa na kauli mbiu " Yesu hu Seba, Taa ya Uhai wa Imani yetu" na hatimaye kuchapicha
matunda ya Sinodi ambayo kwa sasa yanafanyiwa kazi na Familia ya Mungu, Jimbo kuu
la Tabora. Katika mahojiano maalum na Radio Vatican, Askofu mkuu Paul Ruzoka wa Jimbo
kuu la Tabora anazungumzia Ukristo Jimbo kuu la Tabora, amali za Ukristo, Sinodi ya
Jimbo, imani, lakini zaidi sifa za Kanisa mahalia.
Ukristo Jimbo
kuu la Tabora ni matunda ya kazi ya Wamissionari wa Afrika waliofika eneo la Tabora
kunako mwaka 1878. Ukristo ni neema, ni ustaajabivu wa Mungu asiyeridhika tu na kuumba
ulimwengu na binadamu, lakini anayejishusha katika hali ya kibinadamu, ili kumkomboa
mwanadamu kutoka katika lindi la dhambi na mauti.
Jimbo kuu la Tabora katika
maadhimisho ya kumbu kumbu ya miaka 60 tangu lilipotambuliwa kuwa ni Kanisa mahalia
na Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa Watu, yaani tarehe 25 Machi 1953, utume wa
kutangaza, kufundisha na kuwatakatifuza Watu wa Mungu umeendelea kushamiri kwa njia
ya Neno la Mungu na Maadhimisho ya Sakramenti za Kanisa.
Askofu mkuu Ruzoka
anasema imani inadhihirika katika utendaji na kwamba, imani ya Kikristo inapata chimbuko
lake katika haki ya Mungu inayookoa. Anasimulia kwa kina na mapana sifa za Kanisa
mahalia: uongozi; hali ya kujitanua na hatimaye kujitegemea.
Na Padre Richard
A. Mjigwa, C.PP.S. Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.