2015-02-18 10:01:10

Ogopa kifo maji!


Padre Federico Lombardi, msemaji mkuu wa Vatican anabainisha kwamba, Baba Mtakatifu Francisko, Jumanne tarehe 17 Februari 2015 majira ya jioni amekutana na kuzungumza na ujumbe wa Kikosi cha Uokoaji cha Wanamaji kutoka Italia, waliokuwa wameambatana na viongozi wa Serikali ya Italia.

Wanajeshi hao wamemshirikisha Baba Mtakatifu Francisko ushuhuda, changamoto na matatizo wanayokabiliwa nayo wakati wa kutoa huduma ya uokoaji kwa wahamiaji na wakimbizi wanaojikuta wako kwenye Bahari ya Mediterrania, huku wakipambana na kifo! Ujumbe huu wa watu wanane, umesimulia ushuhuda unaogusa undani mwa mwanadamu katika maisha yake, kwa kuona jinsi watu wanavyopambana na kifo maji, jambo la kutisha na kutia huruma.

Baba Mtakatifu, baada ya kusikiliza kwa makini, amewashukuru na kuwapongeza wanajeshi hao kwa niaba ya wenzao, wanaoendelea kujisadaka kwa ajili ya kuwaokoa wakimbizi na wahamiaji wanaotafuta hifadhi ya maisha yao Barani Ulaya, kiasi hata cha kuthubutu kujisadaka katika tumbo la Bahari ya Mediterrania.







All the contents on this site are copyrighted ©.