2015-02-11 08:57:26

Mchakato wa mageuzi!


Baba Mtakatifu Francisko amekuwa akihudhuria mkutano wa Baraza la Makardinali washauri wakuu kuhusiana na mchakato wa mabadiliko katika Sekretarieti ya Vatican. Baraza la Makardinali limeendelea kuchambua Baraza la Kipapa la Utamaduni pamoja na taasisi za mawasiliano ya jamii zinazomilikiwa na kuendeshwa na Vatican.

Mkutano huu kati ya Baba Mtakatifu na Makardinali unafanyika kwenye Hosteli ya Mtakatifu Martha, iliyoko mjini Vatican anasema Padre Federico Lombardi, Msemaji mkuu wa Vatican. Makardinali wamesikiliza taarifa iliyotolewa na Kardinali Gianfranco Ravasi, Rais wa Baraza la Kipapa la Utamaduni kuhusu mapendekezo yake mintarafu magauezi ya Sekretarieti ya Vatican. Baraza la Kipapa la mawasiliano ya jamii pia amewasilisha mapendekezo ya marekebisho kuhusiana na vyombo vya mawasiliano ya jamii vinavyomilikiwa na kuendeshwa na Vatican.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.







All the contents on this site are copyrighted ©.