2015-02-09 08:33:02

Uchaguzi mkuu Nigeria sasa ni 28 Machi 2015


Tume ya uchaguzi nchini Nigeria imeamua kuahirisha uchaguzi mkuu uliokuwa unatarajiwa kufanyika nchini humo tarehe 14 Februari 2015 hadi tarehe 28 Machi 2015 kutokana na kuendelea kushamiri kwa mashambulizi yanayofanywa na Kikundi cha kigaidi cha Boko Haram.

Kutokana na maafa makubwa yanayosababishwa na Boko Haram, nchi tano za Afrika Magharibi, zimeamua kuunganisha nguvu, kwa kuunda kikosi maalum cha kupambana na kikundi cha Boko Haram. Hadi sasa kikosi hiki kina jumla ya wanajeshi 8, 700 kutoka: Benin, Cameroon, Niger, Nigeria na Chad.

Pamoja na juhudi zote hizi, bado Boko Haram kinaendeleza mauaji, jambo ambalo linaendelea kusababisha hofu na mashaka kwa wananchi wengi huko Nigeria.







All the contents on this site are copyrighted ©.