2015-02-05 12:03:44

Askofu mkuu Bruno Musarò, Balozi mpya wa Vatican, nchini Misri


Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu mkuu Bruno Musarò kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Misri na mwakilishi wa Vatican katika Umoja wa Falme za Kiarabu. Kabla ya uteuzi huu, Askofu mkuu Bruno Musarò alikuwa ni Balozi wa Vatican nchini Cuba.

Askofu mkuu Musarò alizaliwa nchini Italia tarehe 27 Juni 1948. Baada ya masomo na majiundo yake ya kikasisi, akapadrishwa kunako tarehe 19 Septemba 1971. Tarehe 3 Desemba 1994 kuwa Askofu na kuwekwa wakfu hapo tarehe 6 Januari 1994. Tangu wakati huo amekuwa ni Balozi wa Vatican nchini: Madagascar, Visiwa vya Comoro, Visiwa vya Seychelles, Mauritius, Guatemala, Perù na mwishoni alikuwa nchini Cuba.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.







All the contents on this site are copyrighted ©.