Baba Mtakatifu Francisko amesema kutafakari injili kila siku , husaidia kujijenga
katika tumaini la kweli. Ni msisitizo aliotoa mapema Jumanne asubuhi wakati akiongoza
Ibada Misa katika Kanisa dogo la Mtakifu Marta la hapa Vatican. Papa amehimiza waamini
kupata muda wa kusoma Injili kila siku hata kwa hata dakika 10 tu, kupata muda wa
kuzungumza na Bwana, badala ya kupoteza muda wote kutazama michezo na maigizo ya wasanii
katika vyombo vya mawasilano au kusikiliza porojo za mitaani muda wote
Papa
alieleza kwa kutazama ni ipi misingi ya matumaini ya Mkristo. Na alitoa jibu kwamba,
ni kuitazama sana sura ya Kristo . Homilia ya Papa ilisonga mbele kwa kutazama kifungu
kutoka Waraka Mtume Paulo kwa Waebrania ambacho kinalenga juu ya matumaini. Papa alitafari
na kueleza kuwa bila kusikiliza sauti ya Bwana,mtu huwa na uwezekano kidogo sana wa
kujenga tumaini kwa yaliyo mazuri zaidi kwa siku za baadaye. Na hivyo akamtaka kila
muumini kujifunza jinsi ya kujiweka chini ya ulinzi wa Yesu, kuwa na matumiani kwa
Yesu. muhimu kufanya "maombi na kutafakarjuu ya neno la Injili na hili linaweza kufanyika,
kwa kuwa na moyo wa kuisoma Injili.
Papa amehoji kwa vipi inaezekana leo hii
kuitafakari Injili ? na kutoa jibu kwamba ni kwa kumweka esu akilini mwetu muda
wote, Kutambua kuwa Yesu yu pamoja na watu wake muda wote. Yesu muda wote akiwa hapa
duniani alikaa kati ya umati wa watu. Na daima alitembea na watu barabara, aliandamana
na watu. Na hata katika usafiri wa maji aliandamana na watu, kama injili inavyosema,
alikuwa amelala juu ya mashua lakini dhoruba alipokuja na wanafunzi wake wakamwamsha.
Na ndivyo inavyotakiwa pia hata siku hizi kutambua kwamba, Yesu yu karibu yetu.
Anasubiri tumwamshe na kumwambia, Bwana dhoruba inatuangamiza, naye atauliza pepo
zote.
Papa aliendelea kutazama somo la Injili ya leo, akisema , Yesu anatambua
kwamba mwanamke mgonjwa katika umati wa watu amemgusa. Tukio hili linatuhimiza kufanya
bidii za kuwa karibu na Yesu, kugusa hata upinde wa vazi lake naye atatuponya. Ni
kufanya kumbukumbu katika njia yote ya mapito ya maisha, na kumbukumbu ya neema nyingi
tulizo pokea kutoka kwa Bwana. Ni kuwa na matumiani na Bwana, ambaye ni mmoja tu,
mwenye uwezo wa kutupa matumaini mapya. Nikumtazama sana Bwana , kumjua Bwana, na
kuitafakari Injili na kusali kwa ajili ya tafakari hii,. Papa ameomba kila mmoja
tangu leo ajaribu kupata muda wa dakika kumi tu, kwa ajili ya kusoma Injili na kufikiria
juu yake na kisha kusema , kila jambo namwachia Yesu.