Wiki la jamii: Wadominicani nchini Angola wasisitiza nafasi sawa kwa wote
Taasisi ya Mosaiko Angola, inayoendeshwa na Watawa Wadomenican, Jumamosi tarehe 31
Januari walikamilisha Wiki la Jamii , na msisitizo wa Fursa Sawa, kwa raia wote wa
Angola. Wiki la Jamii lilianza Jumanne Januari 27 na kumalizika Jumamosi Januari 31,
2015, katika Mji Mkuu wa Luanda. Malengo ya siku hizi tano, ilikuwa ni kutafakari
na kuongeza ufahamu miongoni mwa washiriki, juu ya umuhimu wa majukumu ya kijamii
na kutafuta njia halisi za kushuhudia injili ya Kristo katika dunia ya leo.
Taarifa
kutokea Washiriki wa tukio hili la wiki nzima, imeeleza kuwa kati ya yalijitokeza,licha
ya masuala ya kiroho pia masuala mbalimbali yanayogusa mioyo ya watu katika maisha
sambamba na masuala ya kiroho ikiwa ni pamoja na ukosefu wa fursa sawa katika jamii
, kuanzia sera za Serikali juu ya kukuza usawa kwa wote na usawa wa kijinsia kwa
ujumla; fursa sawa katika matumizi ya rasilimali; demokrasia ya kiuchumi na maendeleo
ya binadamu; mapambano dhidi ya umaskini na dosari zingine katika Angola ya Waangola
, vilevile wajibu wa Kanisa katika uendelezaji wa fursa sawa kwa wote.
Ingawa
Wiki ya kijamii, asili yake ina nia za Kikanisa, lakini limeonekana kuwa kama tukio
wazi la kijamii, ambamo sauti za Waangola wote ziliweza kusikika.
Taasisi Mosaiko,
hulenga kukuza maelewano na kujenga nguzo za ushirikiano wa baadaye ndani ya Angola.
Ilianzishwa mwaka 1997 na wamisionari Dominikani, vikariati ya Angola mara ya kwanza
kama taasisi wasi kwa ajili ya kukuza haki za binadamu nchini Angola. Na kazi zake
hufanikishwa kwa nguvu ya watu kujitolea, katika kueneza heshima kwa utu wa binadamu
na maendeleo ya jamii ya Angola. Ni hasa hulenga katika ufanikishaji wa wananchi
wote wa Angola, kushiriki katika mchakato wa kidemokrasia. Hayo yameelezwa na Bruda
Julio Candeeiro, OP ni mkurugenzi wa sasa wa Taasisi Mosaiko.