Baba Mtakatifu Francisko ameidhinisha orodha ya majina ya wawakilishi wa Mabaraza
ya Maaskofu Katoliki kutoka sehemu mbali mbali za dunia, watakaoshiriki katika maadhimisho
ya kumi na nne ya Sinodi ya Maaskofu kuhusu Familia, yatakayofanyika mjini Vatican
kuanzia tarehe 4 hadi tarehe 25 Oktoba 2015 kwa kuongozwa na kauli mbiu "Wito na utume
wa Familia ndani ya Kanisa na Ulimwengu Mamboleo".
Ifuatayo ni orodha ya majina
ya Maaskofu kutoka Barani Afrika: 1. Burundi: Askofu Gervais Banshimiyubusa, Rais
wa Baraza la Maaskofu Katoliki Burundi na msaidizi wake ni Askofu Joachim Ntahondereye
wa Jimbo Katoliki Muyinga.
2. Ethiopia na Eritrea: Askofu Tsegaye Kenen Derera,
Jimbo Katoliki la Soddo na msaidizi wake ni Askofu Markos Gebremedhin, Jimbo Katoliki
la Jimma Bonga, Ethiopia.
3. Ghana: Askofu mkuu Gabriel Charles Palmer-Buckle,
Jimbo kuu la Accra, na msaidizi wake ni Askofu Anthony Kwami Adanuty, Jimbo Katoliki
la Keta Akatsi.
4. Kenya: Kardinali John Njue, Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki
Kenya; Askofu James Maria Wainaina Kungu, Jimbo Katoliki la Muranga. Msaidizi wake
ni Askofu Emmanuel Barbara wa Jimbo Katoliki Malindi.
5. Madagascar: Askofu
Dèsirè Tsarahazana, Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Madagascar. Msaidizi wake
Jean de Dieu Raoelison, Askofu msaidizi wa Jimbo kuu la Antananarivo.
6. Rwanda:
Askofu Antoine Kambanda, Jimbo Katoliki la Kibungo na msaidizi wake ni Askofu Smaradge
Mbonyintenge, Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Rwanda.
Na Padre Richard
A. Mjigwa, C.PP.S. Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.