Padre Sandro Spriano, Mchungaji wa Kiroho katika gereza Kuu la Rebbibia la Jiji la
Roma hivi karibuni katika mahojiano na Allesandro De Carolis wa Redio Vatican, alieleza
nia ya Kanisa kuendelea kuwajali hata wahalifu waliofungwa gerezani, akisisitiza kwamba
ni muhimu kuwajali wafungwa, kwani kufungwa hakupunguzi thamani ya utu wa mtu.
Na gereza ni mahali na wakati muafaka, ambamo mfungwa anaweza kuona makosa yake
na kwa urahisi pia akipata mwongozo mzuri wa maisha, hasa vijana, huweza kujenga maisha
mapya ya heshima, kwa wengine. Mama Kanisa kupitia kazi zake za Kichungaji katika
magereza, hutazama kwa kina, mazingira wanamoishi wafungwa , na maisha ya gerezani
kwa ujumla, na hitaji la mfungwa mmojammoja, na hivyo kuona kipi kinachotajika zaidi
katika kumsaidia kiroho, kwa ajili ya kubadili mwenendo wake wa maisha. Kwa Makasisi
wanaotoa huduma magerezani, wanahitaji kuifanya kazi hii kwa tahadhari na mshikamano,
ili kumsaidia mfungwa kubadili maisha yake na hivyo kuweza hata kupunguza maisha yake
ya kukaa jela.
Na hivyo, lengo kuu la uwepo wa Makasisi magerezani , ni
kusaidia wafungwa, wote vijana na watu wazima, kuutazama ukweli wa maisha yao ya nyuma,
ili katika ukweli wa yale waliyoyatenda hadi kuwafikisha jela, waweze kuona umuhimu
wa kutoa maamuzi thabati katika kuachana na uovu ambao hauwapeleki mbali kimaisha,
wabadili mwendo huo na kuchukua mwelekeo mpya wa maisha yaliyo bora zaidi yenye kukubalika
kijamii.
Padre Spriano anasema, wao kama makuhani, hutoa huduma yao kwa kadri
ya taaluma yao, na hivyo huwavutia wafungwa wengi, kutafakari juu ya maisha yao. Na
huduma hii ni muhimu kwa Makasisi wote , kwa kuwa iwapo watawanyanyapaaa wafungwa,
basi huduma yao inakuwa sawa na bure. Mfungwa ni mtu mpweke anayehitaji klla kuonyeshwa
njia mpya na kiufarijiwa na wengine, Ni muhimu wafungwa kupata huduma ya kuponywa
kwa faraja za kiroho. Makasisi huanza kazi hii yakubadili maisha ya mfungwa,
kwanza kupitia uwezekano wa mazungumzo ya ana kwa ana, kw akuzingatia kwamba, idadi
kubwa ya vijana na watu wazima hutoka katika kila aina ya maisha , wale waliokuwa.
Kuna wakiishi pembezoni mwa jamii, waliokuwa wakinywa haki msingi za maisha, wale
waliokuwa wamezongwa na umaskini na upweke, na wengine walikuwa katika hali nzuri
lakini wakiishi na moyo wa kutoridhika n.k.. Na hivyo, katika safari hii ya maisha,
Makuhani huanza hasa na njia za kusikiliza matatizo ya wafungwa, na baadaye, kutoa
majibu kwa matatizo hayo kwa njia tofautitofauti kulingana na haja za wafungwa. Ni
jambo la ajabu kwamba wafungwa wengi husikiliza na kuanza kubadili mwelekeo wa maisha
yao wakiwa bado gerezani. Padre Spariano ameeleza huku akiomba sala zaidi kwa
ajili ya ndugu hawa walio magerezani, ili roho zao ziweze kulainika na kumfungua
mlango ili roho wa Kristo, mwenye uwezo wa kuyabadili maisha yao, iwapo watapenda
kwa hiari yao kufanya hivyo, aingie ndani mwao. Na kwamba, Injili haizuii haki za
Mahakama kutendeka kwa mkosaji, lakini husaidia mkosaji kutorudia makosa katika maisha
yake.