2015-01-31 14:47:28

Huduma kwa maskini!


Baba Mtakatifu Francisko ametuma ujumbe wa pongezi na shukrani kubwa kwa Shirika la Misaada la Kanisa Katoliki, Jimbo Katoliki la Mondonedo-Ferrol, lililoko nchini Hispania, kwa kuadhimisha Jubilee ya miaka 50 tangu lilipoanzishwa. Baba Mtakatifu analipongeza kwa kuonesha ushuhuda wa upendo na huduma kwa maskini na wote wanaosukumizwa pembezoni mwa jamii.

Baba Mtakatifu katika ujumbe ulioandikwa kwa niaba yake na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican, anampongeza Askofu Manuel Sanchez Monge pamoja na wajumbe wote wa Caritas Jimboni humo na kuwataka kuendelea kushuhudia huduma ya upendo, inayoonesha neema na upendo wa Mungu kwa waja wake; huduma ambayo ni hai kabisa ndani ya Kanisa.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.







All the contents on this site are copyrighted ©.