Mlipuko wa gari la mafuta wasababisha vifo vya watu 7
Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe wake kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii,
amewakumbuka na kuwaombea wale wote waliofikwa na ajali iliyotokea kwenye Hospitali
ya Watoto mjini Mexico na hivyo kusababisha watu 7 kupoteza maisha yao, kati yao kuna
watoto 3. Baba Mtakatifu anawaombea wote waliofikwa na msiba huu amani na nguvu ya
kuweza kuhimili magumu wanayokabiliana nayo kwa sasa pasi na kukata tamaa.
Taarifa
zinazonesha kwamba, watoto 3 waliofariki dunia ni kati ya watoto wachanga 22 waliojeruhiwa
kutokana na mlipuko wa gari la gesi, uliotokea, Alhamisi, tarehe 29 Januari 2015.
Gari lilikuwa limeegeshwa karibu na jiko, pembeni mwa Wodi ya wazazi, ambako kuna
vitanda maalum kwa ajili ya kutunzia watoto wadogo. Taarifa zinaonesha kwamba, kuna
mtoto mdogo mmoja ambaye ameokolewa kutoka kwenye kifusi cha majengo yaliyobomoka.
Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.