2015-01-26 10:49:08

Pangua pangua ya Rais Jakaya Kikwete Baraza la Mawaziri


Rais Jakaya Mrisho Kikwete wa Tanzania amefanya mabadiliko katika Baraza la mawaziri na kuwaapisha Mawaziri wapya. Katika mabadiliko hayo Raisi Kikwete amemteua muheshimiwa George Simbachawene kuwa Waziri wa nishati na madini, awali alikuwa naibu waziri wa ardhi.

Wengine walioteuliwa ni Dokta Harisson Mwakyembe ambaye amekuwa waziri wa ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, mzee Samweli Sita ameteuliwa kuwa waziri wa Uchukuzi.

Katika mabadiliko hayo pia Rais amemteua mhandisi Christopher Chizza kuwa Waziri wa nchi uwekezaji na uwezeshaji huku Dokta Maria Nagu akiteuliwa kuwa Waziri wa nchi mahusiano na uratibu.

Katika mabadiliko hayo pia Mshemiwa Stephen Wasira ameteuliwa kuwa Waziri wa kilimo, chakula na ushirika huku Williamu Lukuvi akiteuliwa kuwa Waziri wa ardhi nyumba na makazi. Kwa upande wa Naibu waziri, Anne Kilango Malecela ameteuliwa kuwa naibu Waziri wa elimu, Ummy Mwalimu ameteuliwa kuwa Naibu waziri wa Sheria huku Stephen Masele akiteuliwa kuwa Naibu Waziri ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira. Mawaziri hao wanaanza kazi mara moja.








All the contents on this site are copyrighted ©.