2015-01-22 15:32:58

Papa ataja wajumbe wa Taasisi mpya ya kimahakama


Baba Mtakatifu ameteua majina kadhaa ya viongozi wa Kanisa, watakao kuwa wajumbe wa Taasisi aliyoiunda, kwa ajili ya kuchunguza Kesi za madhulumu ya kinjisia, hasa kwa watoto yanayofanywa na watumishi wa Kanisa. Taasis hiyo iko chini ya Shirika kwa ajili ya Mafundisho Sadikifu. Papa alianzisha Taasisi hiyo kwa Barua yake ya kitume ya 3 Novemba 2014, prot. N.62.411.
Walioteuliwa ni Askofu Charles J. Scicluna, Askofu Mkuu wa Jina wa San Leone, Malta, ambaye anakuwa Rais wa Taasisi hiyo.
wajumbe wengine ni Kardinali Zenon Grocholewski, Mkuu wa Usharika kwa ajili ya Elimu Katoliki,
Kardinali Attilio Nicora, Padre Mkuu wa Makanisa ya Mt. Francis na Mt. Maria wa Malaika Assisi:, Kardinali Francis Coccopalmerio, Rais wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Nyaraka Takatifu; Kardinali Giuseppe Versaldi, Rais wa Tume ya Uchumi kwa Jimbo Takatifu; Askofu Mkuu José Luis Mollaghan, Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo Kuu la Rosario; Askofu Juan Ignacio Arrieta Ochoa de Chinchetru, Askofu wa Jina wa Civitate, ambaye ni Katibu wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Nyaraka Takatifu . .
pia kuna wajumbe Mbadala nao ni :Kardinali Julian Herranz, Rais Mstaafu wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Nyaraka Takatifu,; Askofu Giorgio Corbellini, Askofu wa Jina wa Abula, Rais wa Kazi za Kiti Kitakatifu na Tume ya Nidhamu katika ofisi za Curia ya Roma.








All the contents on this site are copyrighted ©.