Papa akutana na ujumbe wa kiekumene kutoka Finland
Baba Mtakatifu Francisko amekutana na ujumbe wa Kiekumene kutoka Finland, kwa kuonyesha
furaha yake na kwa moyo mkunjufu aliwakaribisha na kuwatakia kila la heri katika
hija yao ya kila mwaka hapa Roma, kwa ajili ya kusherehekea sikukuu ya Mtakatifu
Henrik, msimamizi wa Nchi yao. Papa alionyesha kufurahia zaidi kwamba, kwa mwaka
huu, hija hii imekuwa kweli tukio kiroho na kiekumeni , kwa uwepo pia mkutano kati
ya Wakatoliki na Walutheri, tukio ambalo limekuwa likifanyika kila mwaka sasa karibia
miaka 30.
Katika hotuba yake, Papa Francisko, alirejea utendaji huu unaoelekea
kutimiza miaka 30, tangu Makatifu Yohana Paulo II, alipokutana kwa mara ya kwanza
na ujumbe wa kiekumeni kutoka Finland, uliofika hapa Roma, na aliwapokea kwa maneno
haya: "Ukweli ni kwamba, kuja kwenu kwa pamoja hapa Roma, tayari ni ushuhuda umuhimu
katika juhudi za kuwa na umoja . Na Ukweli kwamba, wamekuwa pamoja katika kutolea
Ibada na sala inakuwa ni ushuhuda katika imani yao kwamba, ni tu kwa neema ya
Mungu Wakristo wanaweza kufikia umoja. Na ukweli kwamba, wameweza kuikiri sala ya
Imani kwa pamoja ni ushuhuda wa imani moja kwa kanisa zima la Kristo.
Papa
Francisco amekumbusha kwa kuitaja hatua hii ya kwanza muhimu ya kiekumeni katika
safari kuelekea umoja kamili na ya kuonekana ya Wakristo nchini Finland, lakini pia
akasema, bado kuna mengi ya kufanywa kwa ajili ya kukuza umoja huu wakutembea pamoja
kama Wakristo kuelekea ushirika kamili katika ukweli na upendo kama alivyoandika
Mtakatifu Yohane Paulo II katika waraka wake wa kitume wa Enc Ut unum sint.
Aidha
Papa Francisco, ameifurahia ziara yao wanaoifanya sambamba na Wiki la Maombi kwa
ajili ya Umoja wa Kikristo, ambalo kwa mwaka huu, linaongozwa na Yesu alizungumza
kwa mwanamke msamaria kisimani: "Nipe kinywaji" (Yoh 4,7). Papa Francisco anasema,
tukio hili, linatukumbusha kuwa, chanzo cha neema zote ni Bwana mwenyewe, na kwamba
ni zawadi yake yenye kuleta mabadiliko katika maisha kwa wale ambao hulipokea Neno
na kutoa maamuzi ya kuliisho, wanakuwa mashahuda wa maisha halisi ambayo huja tu
kutoka kwa Kristo. Kama Injili inavyo sema, Wasamaria wengi walimwamini Yesu kwa ushuhudi
wa mwanamke Msamaria . Papa Francisco pia alitaja kama alivyobaini Askofu Vikström,
Wakatoliki na Walutheri unaweza kufanya mengi kwa pamoja, katika kuishuhudia huruma
ya Mungu katika jamii yetu. ushuhuda wa pamoja wa Kikristo, unahitaji kuonekana hasa
katika uso wa kutoaminiana, uso wa ukosefu wa usalama, mateso na madhulumu, na utendaji
mbovu wa watu wengi katika dunia ya leo.
Papa ameendelea kuzungumzia ushuhuda
huu pamoja kwamba, , unaweza kuungwa mkono na kuhimizwa na kusonga mbele kwa majadiliano
ya kiteolojia kati ya Makanisa. Na Azimio la Pamoja juu ya mafundisho ya kuhesabiwa
haki, lililotiwa saini rasmi zaidi ya miaka kumi na tano iliyopita kati ya Shirikisho
la Dunia la Waluteri,na Kanisa Katoliki la Roma, vinaweza kuzaa matunda zaidi ya maridhiano
na ushirikiano.