2015-01-22 13:50:22

Maisha ni zawadi!


Baraza la Maaskofu Katoliki katika mchakato unaopania kukuza na kudumisha Injili ya Uhai, tarehe 22 Januari 2015, linakumbuka miaka arobaini na mbili tangu Mahakama kuu nchini Marekani ilipopitisha sheria ya utoaji mimba, kunako mwaka 1973.

Tangu wakati huo, Familia ya Mungu nchini Marekani, inaungana kwa pamoja kwa ajili ya kufanya novena, kufunga na kusali kwa ajili ya kuenzi Injili ya Uhai. Huu ni muda muafaka kwa kuonesha mshikamano na Kanisa zima, ili kutangaza Injili ya Uhai na Familia kwa njia ya ushuhuda wa imani tendaji!

Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe wake kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii anakazia kwamba, maisha ya kila binadamu ni zawadi kubwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu, inapaswa kulindwa, kutunzwa na kuendelezwa.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.







All the contents on this site are copyrighted ©.