Baba Mtakatifu Francisko, ameomba amani na mapatano kwa taifa la Niger, kufuatia mashambulizi
ya hivi karibuni yaliyofanywa na kikundi cha Boko Haram. Papa ametoa wito huo, baada
ya kukamilisha katekesi yake kwa mahujaji na wageni waliokusanyika katika ukumbi wa
Paulo VI wa hapa Vatican, mapema Jumatano hii.
Papa ameomba watu wote wenye
mapenzi mema, kuombea mema taifa pendwa la Niger, na hasa kafara wa upinzani uliofanywa
na kikundi cha Boko haram hivi karibuni nchini humo, madhulumu makubwa yaliyolegwa
kwa Wakristo, watoto na makanisa. Na amemwomba Bwana, zawadi ya mapatano na amani
ili kwamba dini kamwe isitumiwe kama chombo cha kuzua ghasia, maonevu na uharibifu.
Na amekemea vikali kutumia jina la Mungu, kama sababu ya kuzua vita. Papa anatumaini
amani na utulivu, vitarejea na kudumishwa Niger katika hali za kuheshimiana na kuishi
pamoja kwa ajili ya manufaa ya wote. Na ametolea sala kwa Mama Bikira Maria, Malkia
wa Amani kwa ajili ya watu wa Niger.
Wiki iliyopita, katika mji Mkuu wa Niamey,
na mji wa Zinder , jumla ya watu 15 waliuawa na makanisa kadhaa kuchomwa moto na
kuharibiwa katika ghasia zilizofanywa kikundi cha Kiislamu cha Boko Haramu, wakipinga
picha za katuni zilicho chorwa na gazeti la Charlie la Ufaransa, zinazomwonyesha mtume
Mohamed.Ghasia zilizodumu muda wa siku mbili.
Taasisi za usalama za Niger
, zililazimika kuingilia kati kwa kutumia mabomu ya kutoa machozi kutawanya mamia
ya watu waliojiunga katika uharifu huu ukiongozwa na kikundi cha Boko haramu.