2015-01-20 10:07:45

Marehemu Askofu Zuza, atakumbukwa na wengi!


Askofu mkuu Julio Murat, Balozi wa Vatican nchini Malawi na Zambia, Jumatatu tarehe 19 Januari 2015 ameongoza Ibada ya Misa takatifu kwa ajili ya kumsindikiza katika usingizi wa amani, Marehemu Askofu Joseph Mukasa Zuza, aliyefariki kwa ajali ya gari hivi karibuni nchini Malawi. Marehemu Askofu Zuza amezikwa kwenye Kanisa kuu la Mtakatifu Petro, Jimbo Katoliki Mzuzu, Malawi.

Marehemu Askofu Zuza aliyekuwa pia Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Malawi na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Malawi, atakumbukwa na wengi kutokana na ujasiri wake, uliosaidia mchakato wa maendeleo endelevu ya wananchi wengi wa Malawi.

Alikuwa ni kiongozi mwenye fadhila ya uvumilivu; mkarimu na mpole na mwelewa, aliyetumia karama na mapaji yake kupambanua mambo kwa ajili ya mafao ya wengi; anasema Rais Peter Mutharika wa Malawi. Atakumbukwa na wengi kama kiongozi aliyejisadaka kwa ajili ya maendeleo na mafao ya wananchi wa Malawi.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.
Kwa msaada wa Wakala wa Habari za Afrika CANAA.







All the contents on this site are copyrighted ©.