Mpendwa Msikilizaji wa Kipindi chetu cha Kanisa la nyumbani, Tumsifu Yesu Kristo!
Karibu kwa mara nyingine tena tuendelee kufikiri na Kanisa kwa njia ya ujumbe wa hati
za Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vaticani. 00:10:33:41
Leo tunaitazama
hati ile inayohusu upyaishwaji wa maisha ya Kitawa inayojulikana kwa jina la Kilatini
Perfectae Caritate, ikimaanisha Mapendo Kamili. Hati hii inatoa maelekezo ya jumla
kwa watawa na maisha ya kitawa ndani ya Kanisa, kwa lengo la kuwafanya watawa na utume
wao viendani na fikra za Kanisa na mahitaji ya mazingira.
Tufahamu kwamba,
utawa ni mfumo wa maisha ndani ya Kanisa ambamo, baadhi ya wabatizwa waume kwa wake,
huitwa na Mungu na kuishi maisha ya kitawa kwa kufuata mashauri ya Injili, huku wakiongozwa
na Upendo kwa Mungu na jirani, dhana inayojionesha katika maisha na huduma yao kwa
Kanisa na Ulimwengu. Ni kwa namna hiyo, tunaona kwamba kiini haswa cha maisha na utume
wa Mtawa ni kujishikamanisha na Mungu ili kuweza kuyatakatifuza malimwengu. Watawa
wanayatakatifuza malimwengu kwa njia ya Mfano wa maisha yao ya kujisadaka, kwa njia
ya sala zao na huduma zao, huku wakiufuasa mfano wa Kristo mwenyewe aliyekuja si
kutumikiwa bali kutumikia.
Kwa mujibu wa taratibu zetu, mbatizwa yeyote, mwenye
kujisikia wito wa utawa huweza kujiunga na shirika lolote la Kitawa. Kuna aina mbalimbali
za mashirika ya kitawa ndani ya Kanisa. Kuna mashirika yanayoshughulika na kusali
tu katika na u; kuna mashirika yaliyoanzishwa ili kutimiza huduma maalumu kwa niaba
ya na kama sehemu ya maisha yao ya kitawa; pia kuna mashirika yanayotakiwa kuunganisha
kiaminifu ratiba ya sala na taratibu nyingine za kijumuia pamoja na fulani.
Kuna
mashirika ya kikleri na mashirika ya kilei. Yapo mashirika ya watawa wa kiume tu (pasipokuwa
na mapadre ndanimwe), kuna mashirika ya kitawa ya kike na kuna yanayotafuta kwa
kuishi katika mazingira ya kawaida ya watu, pasipo kujitenga na kwenda kuunda jumuiya.
Mashirika
hayo yote yanaongozwa na Karama maalum ya mwanzilishi na watawa huiishi Karama hiyo
kama inavyotambuliwa na Kanisa. Na watawa hao hujishikamanisha na maisha hayo kwa
vifungo vya nadhiri zenye msingi katika mashauri ya Injili au vifungo vingine vitakatifu,
lengo likiwa ni kumtafuta Mungu kwa njia ya kumfuasa Kristo kwa ukaribu zaidi kwa
njia ya kuyaishi mashauri hayo ya Injili.
Hao wote wanamfuasa Kristo yule
yule. Wapo wanaomfuasa Kristo anayesali, wapo wanaomfuasa Kristo anayefundisha, wapo
wanayemfuasa Kristo anayeponywa wagonjwa, wapo wanayemfuasa Kristo anayehubiri Habari
Njema ya Ufalme wa Mungu, wapo wanaomfuasa Kristo anayewatendea mema watu, na wapo
wanaomfuasa Kristo anayeshiriki maisha ya watu. Ni kwa mtazamo huu ndio tunakuta kuwa
tuna mashirika mengi yenye karama tofauti-tofauti ndani ya Kanisa. Watawa wote kwa
njia ya huduma zao, wanachangia katika maisha, usitawi na utakatifu wa Kanisa.
Ni
kwa sababu ya uzito huo wa maisha ya Kitawa, Mtaguso Mkuu uliona ni vema ukayapatia
maisha ya kitawa mwongozo kamili, ili maisha hayo ya kitawa yapate maana chanya zaidi
ndani ya Kanisa. Mtaguso ulisisitiza hali mpya ya inayopaswa kuonekana katika mambo
makuu matano yaani: kushika kama kuu, kufuata kiaminifu ya na bora ya , kujihusisha
na maisha na malengo yote ya Kanisa, kupima hali na mazingira ya watu wa leo, kuweka
mbele kuliko mambo mengine. Ni kwa mtazamo huo tu, ndio watawa wataweza kumwilika
katika Kanisa na mazingira na nyakati halisi.
Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican
uliwahimiza watawa kushika , kujikatalia malimwengu, kujiwekwa kwa juu ya msingi
wa , kulitumikia Kanisa, kutekeleza , kumfuata kwa bidii kama jambo pekee na la
lazima, na kuunganisha maisha ya na moyo wa kitume. Kupenda kufanya kazi ndani ya
Kanisa na kwa ajili ya Kanisa, kwani mashirika yote ya Kitawa ndani ya Kanisa ni mali
ya Kanisa, ni mikono ya Kanisa. Hivyo utume wowote ulenge katika kushiriki kazi ya
Kanisa ya kumkomboa mwanadamu kiroho na kimwili.
Mpendwa msilikizaji wa Kipindi
chetu cha Kanisa la Nyumbani, tunakuletea habari hii sasa ambapo Kanisa linaadhimisha
Mwaka wa Watawa. Pamoja na mambo mengi ambayo tumefunzwa kuhusu watawa, na sisi kwa
upande wetu tuone mambo mawili tu. Kwanza tujibidishe kuyaenzi maisha ya kitawa. Katika
uhalisia wake, wengi wetu tumeona na tunathamini na tunahitaji kabisa huduma za watawa.
Lakini neno ni lilelile. Watawa ni watoto wetu, wanaitwa kutoka katika familia zetu
kwa ajili ya kutuhudumia sisi wenyewe.
Basi, tujibidishe sote katika kulea
vizuri watoto wetu ili katika akili tulivu na dhamiri hai, waweze kuisikia sauti ya
Mungu anayewaita. Hati hii inasema kuwa jukumu la kulea miito ni la wazazi, watawa
wenyewe kwa njia ya mfano wa maisha yao, pamoja na wachungaji wetu wa Kiroho. Sisi
wanafamilia, tulizawadie Kanisa letu watawa, ili kazi ya Injili isonge mbele zaidi.
Wakati
fulani huwa kunakuwa na wazazi wa ajabu sana, ambao wanapenda sana watawa, na wanapenda
watoto wao walelewe na wasome shule za watawa! Na wanastaajabia huduma zinazofanywa
na watawa ndani ya Kanisa. Lakini wakisikia kuwa mtoto wao ana wito wa utawa, wanafanya
kila aina ya fatiki ili kumkatisha tamaa kupindisha mawazo hayo kwa mtoto huyo. Wapo
wazazi na walezi waliomdhulumu Mungu anayeita watu na kulikosesha kanisa Watenda kazi,
kwa kuwakataza kabisa watoto wao wasijiunge na maisha ya kitawa.
Pili, kwa
mwaka huu tunapoadhimisha Mwaka wa Watawa, waamini wote katika ngazi zote, tuone namna
ya kuwashukuru watawa kwa majitoleo yao kwa Kanisa. Namna ya kwanza ya kuwashukuru
ni kuwaombea wadumu katika wito wao. Na ya pili ni kuwapa ushirikiano katika utume
wao, ya tatu ni kuwalinda wasipatwe na mabaya. Nyakati fulani na katika mazingira
fulani watawa wetu wanateswa kweli. Hata kama wapo kwa ajili yetu, wanatuhudumia afya
zetu, utashangaa sisi wenyewe ndio tunawapiga, tunawaibia vifaa vya kazi, tunawadhulumu
haki zao na mambo kama hayo.
Hapa swala la msingi ni hili: endapo watawa wapo
katika maeneo yetu wanatutumikia, sisi watu wa maeneo hayo tuwalinde ili wakae kwa
usalama. Na wanapotutumikia, tuwape malipo ya haki, bila kusahau kuchangia matunzo
yao uzeeni, ili wasizeeke kwa huzuni baada ya kazi ngumu ya kuwahudumia watu. Tuwajengee
watawa wetu mazingira ya amani, ili waishi na kumtumikia Bwana kwa furaha na kwa njia
ya huduma zao Mungu Atukuzwe, Ulimwengu Utakaswe na sisi tuokolewe.
Kutoka
katika Studio za Radio Vatican, ni Mimi Padre Pambo Martin Mkorwe, OSB.