2015-01-12 12:12:39

Boko Haram inatisha!


Askofu mkuu Ignatius Kaigama, Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Nigeria anasema kwamba, kwa sasa mashambulizi yanayofanywa na Kikundi cha kigaidi cha Boko Haram nchini Nigeria yanatisha na kufedhehesha sana, kwani watu wanauwawa kikatiliki, kiasi hata cha kuwatumia watoto wadogo kwa ajili ya mashambulizi ya kujitoa mhanga!

Askofu mkuu Kaigama anasema, watu wengi wanaendelea kusikitishwa kutokana na mauaji ya watu wasiokuwa na hatia, wanajiona kuwa hawana uhakika wa usalama wa maisha na mali zao, daima kifo kinawanyemelea wakati wowote. Kikundi cha Kigaidi cha Boko Haram kinaendelea kujitanua na kujiimarisha wakati wanasiasa wanapiga kampeni za uchaguzi mkuu, kana kwamba, hakuna kinachoendelea nchini Nigeria. Kikundi hiki kinashikilia maeneo nyeti na baadhi ya watu wametekwa nyara na wanalenga kujitanua hadi Cameroon, Chad na Niger.

Katika mazingira kama haya, Askofu mkuu Kaigama anawaalika watu wenye mapenzi mema kuendelea kuwakumbuka katika sala na sadaka zao, wakati huo huo, Jumuiya ya Kimataifa ijipange vyema, ili kusaidia mchakato wa kupatambana na Kikundi cha kigaidi cha Boko Haram, ili haki, amani na utulivu viweze kurejea tena nchini Nigeria.







All the contents on this site are copyrighted ©.