2015-01-10 10:48:50

Wafukuzwa kwa kukataa kukana Ukristo - Mosul Iraki


Wazee kumi Wakaldayo Wakristo Wakatoliki wa Syria , wamefukuzwa kutoka eneo lao na Wanamgambo wa kujitegemea wanajihadi wa Kiislam, waliozingira vijiji katika uwanda wa Ninawi Iraki. Katika eneo hilo, kuna makazi ya pili kwa ukubwa la watu wanaokimbia ghasia na mauaji yanayofanywa na wanajihadi hao.Wazee hao walipewa amri ya kuondoka mara moja, baada ya kukataa kuikana imani yao ya Kristo, wakitakiwa kuongokea Uislamu.

Wazee hao walikumbwa na mkasa huo wa kufukuzwa siku ya Jumatano,licha ya baadhi yao kuwa katika hali mbaya za afya. Wazee hao wamepokelewa katika kambi ya Kirkut, baada ya mwendo wa siku mbili katika hali ya baridi na bila kukutana na mtu yeyote na hawakuwa wamechukua kitu chochote cha kuwafadhili kwa kuwa hawakuruhusiwa kufanya hivyo na askari hao wanajihadi, waliojitangazia himaya yao ya kiislamu katika eneo walilolitwaa la Ukrudi ya Peshmerga.


Mmoja wa wazee hao ameshuhudia kwamba , baada ya mwendo mrefu na uchomvu mwingi, hatimae walipata msaada wa kutoka familia ya kiislamu iliyowafadhili kwa chakula na mahitaji mengine muhimu. Wazee hao wametoa shukurani zao kwa Patriaki Raphael Louis Sako, kwa kuiomba serikali ya kiraia, iondoe vipingamizi kwa wazee, wanaopenda kuingia Kirkut kwa sababu za kiusalama . Pamoja na wazee 10 , pia ilikuweko familia moja ya Kiislam.








All the contents on this site are copyrighted ©.